CBWSOs TANGANYIKA WAASWA KUSIMAMIA SHERIA

Mkuu wa Wilaya ya Tamganyika Onesmo Buswelu akiwa katika ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa vyombo vya watoa Huduma ya Maji ngazi ya Jamii.

Na Walter Mguluchuma.

Katavi,

Wadau wa Maji na Mazingira  Katika wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi  wameaswa kusimamia sheria ya huduma ya Maji na usafi wa mazingira namba 5 ya Mwaka 2019 ili kulinda vyanzo vya maji na mazingira ili  kukabiliana na tatizo la uhalibifu wa  vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla .

Baadhi ya watumishi wa wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini Ruwasa Wilaya ya Tanganyika wakiwa katika mkutano mkuu wa Mwaka wa watoa huduma ya Maji ngazi ya Jamii.

Wadau wa Maji na Mazingira  Katika wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi  wameaswa kusimamia sheria ya huduma ya Maji na usafi wa mazingira namba 5 ya Mwaka 2019 ili kulinda vyanzo vya maji na mazingira ili  kukabiliana na tatizo la uhalibifu wa  vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla .

Wito huo  umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika  Onesmo  Buswelu  wakati  akifungua   mkutano mkuu wa mwaka  wa  vyombo  vya watoa huduma  ya    Maji  ngazi ya  jamii(CBWSO) uliofanyika katika ukumbi wa Katavi Resort.

Buswelu  ameeleza kuwa endapo sheria hiyo   Namba  5 ya mwaka 2019 itasimamiwa ipasavyo itasaidia kulinda vyanzo vya maji  na mazingira na  kuimarisha  mfumo  wa utoaji  huduma   za maji safi  na salama pamoja na kulinda mazingira .

Ameyataja  mafanikio yatakayotokana na  sheria hiyo kuwa ni pamoja na  kuimarika  kwa ujenzi  ,usimamizi  na uendeshaji  wa miradi  ya maji  kufuatia  kuundwa  kwa wakala  wa Maji  na usafi  wa Mazingira  Vijijini(RUWASA)  na  kuongezeka kwa  ufanisi  na uwajibikaji  katika  uutoaji wa huduma .

Aingick Trailshoo Msimamizi wa watoa huduma ngazi ya Jamii wilaya ya Tanganyika akisema neno kwenye Mkutano huo

Pia kuwepo  kwa  uendelevu  wa miradi ya maji  Vijijini  kutokana  na kuboreshwa  kwa  muundo  na usimamizi  wa vyombo vya  watoa huduma  ya maji ngazi ya jamii na kuwepo  kwa uendelevu  wa huduma  za maji  hivyo kutachochea  utendaji  katika sekta nyingine  na kuongeza  mchango  wa sekta  ya maji  katika ukuaji  wa uchumi

Kuondoa  mogogoro ambayo imekuwa ikitokea kwenye baadhi ya maeneo mbalimbali  katika jamii zetu hususani  na huduma  za  usimamizi  wa miradi mbalimbali ya maji   inayokuwa inatekelezwa .

 Buswelu  amewaonya watoa huduma  ya maji ngazi ya  jamii  kujiepusha na  Rushwa wakati wanapokuwa wanawahudumia watu maji  na badala yake wanatakiwa kuwa elimisha watumia maji juu ya kulinda miundombinu hiyo ya maji dhidi ya hujuma.

Amefafanua kuwa ipo miradi kwenye Wilaya ya Tanganyika ambayo inaendelea kutekelezwa na mingine imeisha  kamilika  hivyo wanao wajibu  wa kuwahamasisha watu waunganishiwe maji  kwani kwa sasa  kwenye Wilaya hiyo huduma za maji zimeboreshwa  kutokana wananchi kuunganishiwa maji .

 Mwakilishi wa  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tanganyika  Frenk Kibigas ambae ni Diwani wa Kata ya Ntongwe amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya ulipaji wa  bili za maji husunani  kwa  idara za  Serikali kwenye maeneo ya  huko   vijijini.

Ameshauri kuwa  kuanzia sasa bili zote za maji kwenye  maeneo ya  Vijijini   ziwe wanakabidhiwa  Madiwani wa Kata husika ambao  watafanya kazi ya kufatilia  ili taasisi ambazo  zinadaiwa  ziweze kulipa  madeni hayo .

Kwa upandewake kaimu Meneja wa Ruwasa wilaya ya Tangayika  Yeremia  Malisho amesema kuwa Ruwasa wataendelea kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Tanganyika hasa wanao ishi maeneo ya vijijini wanapata huduma ya Maji.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages