PAKA NA MBWA KUPIMWA CORONA




Na Mwandishi Wetu KTPC

Paka na mbwa katika mji mkuu wa Korea Kusini wataanza kupimwa Covid-19 kama wataonesha dalili, mamlaka ya Seoul imesema.

Hatua hii imekuja wiki chache baada ya taifa hilo kuripoti kisa cha kwanza cha mnyama kuwa na Covid-19 - na mnyama huyo alikuwa paka mdogo.

Ni wanyama wa nyumbani pekee wenye kuonesha dalili kama ya kushidwa kupumua vizuri ndio watapimwa corona.

Wanyama hao lazima watengwe nyumbani kama wakikutwa na maambukizi ya virusi vya corona. Si lazima kuwapeleka wanyama hao katika eneo la kujitenga kwasababu hakuna ushaidi kuwa maambukizi ya Covid-19 yanaweza kusambaa kutoka kwa binadamu kwenda kwa wanyama, Park Yoo-mi, afisa wa kudhibiti magonjwa alieleza kikao, kwa mujibu wa ripoti ya Yonhap.

Lakini kama mmiliki wa wanyama hao atakuwa amekuwa amelazwa hospitalini kutokana na Covid-19, au wagonjwa sana na hawawezi kuwaangalia , basi wanyama hao watapelekwa katika eneo la kujitenga.

Nchini Korea Kusini , wagonjwa wa Covid-19 huwa wanatengwa katika eneo maalum kama hawahitaji huduma ya hospitali.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages