ADP MBOZI WASHIRIKIANA NA  NONDO INVESTORS KUTOA MAFUNZO MAALUMU KWA MAAFISA KILIMO KATAVI.



Mratibu wa ADP-Mbozi Mkoa wa Katavi,Edward Mwakagile(aliyesimama) akitoa mafunzo ya kilimo biashara kwa maafisa kilimo pamoja na wakulima viongozi wa kata mbalimbali za manispaa ya Mpanda,halmashauri ya wilaya ya Nsimbo na Tanganyika Mkoa wa Katavi.

Na Mwandishi wetu KTPC,Katavi.

Shirika la ADP Mbozi kwa kushirikiana na Nondo investors limeendelea kutoa mafunzo ya kilimo biashara (Farm business school) kwa maafisa kilimo  na wakulima viongozi   wa kata mbalimbali za manispaa ya Mpanda,Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika na Nsimbo Mkoa wa Katavi

Mafunzo hayo yametokana na wakulima wengi wa mkoa wa Katavi kujishughurisha na kilimo cha mazoea bila kuzalisha mazao kwa tija,ambapo kama watafanya kilimo biashara kitachangia ukuaji wa uchumi wao binafsi,kaya pamoja na jamii nzima.



Kaimu Katibu Tawala-Uchumi na Uzalishaji wa Mkoa wa Katavi,Agustine Mathias(aliyesimama) akiwaleza jambo washiriki wa mafunzo ya kilimo biashara.

Edward Mwagalile,Mratibu wa shirika la ADP Mbozi Mkoa wa Katavi amezungumza hivyo kwenye ukumbi wa ofisi hiyo wakati wa ufunguzi wa semina ya siku nne  iliyohudhuriwa na mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Katibu Tawala –Uchumi na Uzalishaji wa Mkoa wa Katavi,Agustine Mathias.

Mwakagile ameeleza kuwa semina ya  darasa la kilimo biashara litawasaidia wakulima  kupata elimu itakayo wapa wigo mpana wa namna gani  wazalishe kibiashara,namna gani waendeshe kilimo kibiashara,namna gani wazalishe mzao kibiashara,namna gani waongeze faida katika biashara pamoja na wapate uelewa ni namna gani watafanya nini kwenye kilimo.

“…ili kuzalisha mchele ulio bora ambao unaweza kupambana kwenye soko la dunia inampasa mkulima kufahamu afanye nini kwenye kilimo kwa maana kwanini ulime mpunga na sio mahidi,kwanini ulime mboga mboga na sio korosho ambayo yote hayo huwezi kuyaamua kama hujapata elimu kilimo biashara” alisisitiza Mwakagile..

Aidha ameelezea mradi wa Rice SMs-Katavi ambao utadumu kwa mwaka mmoja na nusu ambapo kufikia Decemba mwaka huu utakamilika ukiwa unafadhiliwa na Kilimo Trust ukiwa umejikita zaidi kwenye uzalishaji wa zao mpunga bora sambamba na mchele safi na bora kwa ajili ya kupambana kwenye soko la dunia.

Hivyo amesisitiza mafunzo hayo yanawahusu wakulima,wasindikaji pamoja na mafunzo yanayowahusu walaji ambapo maafisa kilimo  na wakulima viongozi   wako kwa niamba yao ili wakawe mabalozi wa kuwafundisha wakulima vijijini.


Mratibu wa mradi wa Rise SMs-Katavi na Nondo investors,Barick Ngala (aliyesimama)akieleza jambo kwenye mafunzo hayo

Barick Ngala,Mratibu wa mradi wa Rise SMs-Katavi pamoja na Nondo Investors amesema kuwa malengo ya mradi huo ni kuongeza ushindani wa mchele wa mkoani hapa kupitia masoko rasmi na agalau kuwafikia wakulima wadodo 10,500 kwa kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga katika manispaa ya Mpanda,Nsimbo  na Tanganyika.

Ngala alieleza  malengo mengine ni kuongeza mchango wa usambazaji wa mchele kwenye masoko ya ndani na nje kutoka tani 2,400 hadi 9,500 kufikia mwaka huu,kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga kwa wakulima wadodo kutoka tani 2.5 hadi 3.5 kwa kilimo cha umwagiliaji.

“…lengo jingine tunahakikisha tunaongeza upatikanaji wa huduma za kifedha angalau kwa wakulima wadogo 3,000 na wajasiliamali wadogo kufikia 2021” aliongeza Ngala.


Baadhi ya washiriki wa mafunzo wa kilimo biashara walihudhuria mafunzo hayo.

Maeneo ya utekelezaji wa mradi huo utahusisha Wilaya ya Tanganyika kwenye kata za Sibwesa na Mnyagala,Mpanda Manispaa kwenye kata za Kakese na Mwamukulu pamoja na Halmashauri ya Nsimbo katika kata ya Itenka,Huku jumla ya vijiji ambavyo vinafikiwa na mradi kutoka kwenye halmashauri zote tatu ni 12.

Kaimu Katibu Tawala-Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Katavi Augustine Mathias akifungua semina hiyo alilisitiza washiriki kuwajibika katika kuwahudumia wakulima pindi watakapo maliza mafunzo hayo maalumu.

Mathias amesisitiza kuwa serikali inafurahishwa na mashirika kama ADP-Mbozi pamoja na Nondo Investors kuwajibu kwa wakulima katika kuwaongezea uwezo wa kilimo utakao saidi kujikwamua kiuchumi.

Leya Muhando,Fundi Sanifu Kilimo Kata ya Itenka Halmashauri ya Nsimbo amesema kuwa mafunzo hayo rejea wanayoyapata watakwenda kuwakumbusha wakulima na jamii kwa ujumla kuhakikisha usalama wa chakula unakuwepo.

Fundi Sanifu huyo amefafanua kuwa wakulima watawaeleza ni mbinu gani watumie ili kuzalisha mazao yenye tija `ili kuendana na uongezeko la watu.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages