Na Mwandishi Wetu KTPC,Mpanda.
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamewatembelea wanafunzi wenye uhitaji maalumu na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali ya kujikimu pamoja na kuwatia hamasa ya kusoma kwa bidii.
Hayo
yamefanyika kuelekea maadhimisho ya kutimiza miaka 44 ya ccm ambapo
walitembelea shule ya msingi Azimio na shule ya sekondari Rungwa zilizopo
manispaa ya Mpanda Mkoani hapa.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Manispaa ya Mpanda,Azizia Self (wa tatu kushoto) akitoa dumu la mafuta ya kula kwa shule ya Msingi Azimio manispaa hapo yenye watoto wenye mahitaji maalumu. |
Fuljensia
ameleza kuwa kama wanawake wameona kunaumuhimu mkubwa wa kuwasaidia wanafunzi
hao kwa sababu ni sehemu ya jamii ambayo inapaswa kuhudumiwa kwa kila kitu ili
kufanikisha ndoto za wanafunzi hao.
‘’ naiomba jamii ya mkoa wa Katavi kutambua kuwa inawajibu wa kuhakikisha watoto ambao ni walemavu wote wanapatiwa haki ya kupewa elimu…kuwaficha watoto wenye ulemavu ni kitendo kimepitwa na wakati hivyo tuwapeleka na tujitolee kuwa hudumia kila wakati’’ alisema Mwenyekiti huyo.
Mwl Joseph
Fortunatus,Mkuu wa kitengo cha wanafunzi wenye uhitaji maalumu katika shule ya
msingi Azimio,Akipokea mahitaji hayo licha ya kuishukuru UWT pia ameishukuru
serikali kwa kuendelea kuwahudumia wanafunzi hao kwa kuwapatia chakula bure.
Aidha alisema
kuwa bado wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu,uchache wa vifaa vya kufundishia wanafunzi wenye mahitaji maalumu,Uhaba wa
vyumba vya madarasa pamoja na kukosekana kwa jiko la kupitia chakula.
Baaadhi ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi Azimio Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi |
Aisha Juma,Katibu
wa UWT Mkoa wa Katavi amesema licha ya kutoa mahitaji hayo na kukubali kushughurikia
baadhi ya changamoto hizo kwa kuishauri serikali kufanya maboresho kwenye shule
hiyo pia alisema wataendelea zaidi kuhamasisha na taasisi zingine ili kusaidia
wanafunzi hao.
Vilevile
Katibu huyo amesema kuwa wamefanikiwa kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa
wanafunzi wa sekondari Rugwa ili kuwawezesha kujitambua na kuepukana na mimba
za utotoni ambazo kwa kiasi kikubwa zimeshuhudiwa mkoani Katavi.
Katibu huyo
amesema kuwa ni jambo ambalo haipendezi kwa mkoa kushika nafasi za juu kwenye
mimba za utotoni,Hivyo kama UWT wanawajibu wa kuwapa elimu ya afya ya uzazi kwa
vijana wote pamoja na kuwahimiza wazazi
na walezi kusimama kwenye nafasi zao za kuwalinda watoto dhidi ya mimba ambazo
zinauwa ndoto zao.
UWT katika maadhimisho hayo wameandaa huduma ya utowaji wa damu kwa kushirikiana na wataalamu wa huduma ya afya kutoka hosptali ya rufaa Mkoa wa Katavi.