Na Mwandishi Wetu KTPC,Katavi.
Umoja wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya
ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wamefanikiwa kupanda miti mia tatu katika maeneo
mbalimbali ya mkoa huo kwa ajili ya kujenga ustawi wa mazingira na kutunza uoto
wa asili.
Upandaji wa miti huo umefanywa kuelekea maadhimisho ya kufikisha
miaka 44 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo kuelekea kilele hicho,Jumuiya hiyo imeamua kupanda miti.
Kaimu Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi
Mkoa wa Katavi,Hassan Tindo akizindua jana zoezi la upandaji miti katika
viwanja vya Hosptali Teuli ya Rufaa ya Mkoa huo na kuongozwa na mgeni rasmi na
mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Beda Katavi amesema kuwa kama wazazi
wanawajibu kutunza mazingira ili yawe rafiki kwa watu.
Kamishina wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,ACP Benjamin Kuzaga akipanda mti aina ya mwembe katika hosptali ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika. |
Tindo amesema wamefanikiwa kupanda miti katika Hosptali
ya rufaa ya Mkoa wa Katavi,Viwanja vya shule ya msingi Mapinduzi ambapo
zitajengwa nyumba za watumishi wa Chama,Hosptali ya Halmashauri ya Wilaya ya
Nsimbo na Tanganyika,Ofisi Kuu ya CCM Mkoa pamoja na shule ya Sekondari Milala iliyopo
Manispaa ya Mpanda.
‘’…tumepanda miti hii katika maeneo yote haya ni sehemu
ya utekelezaji wa maagizo kutoka makao makuu ya chama cha mapinduzi
tunapoelekea maadhimisho ya kufikisha miaka 44 ya chama chetu pamoja na kupanda
miti hii pia tumeweza kugawa miti zaidi ya 100 kwa wananchi wa mkoa wetu’’
alisema Tindo.
Beda Katani ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM) mkoa wa Katavi wakati wa upandaji wa miti amesema kuwa wananchi
wanawajibu wa kupanda miti kwani maisha ya mwanadamu yanategemea miti kwa kuwa
miti ni uhai.
Katibu wa Chama Cha Waadishi wa Habari Mkoa wa Katavi (KTPC),Paschal Katona (kulia)akipanda mti aina ya mwembe katika hosptali ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika. |
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amesema kuelekea maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa CCM,Kama mkoa wamefanya juhudi kubwa kuwahaudumia wananchi kwa nguvu zote kwani kwa kufanya hivyo wamefanikiwa kupata matunda ya wananchi kukiamini chama hicho sambamba na kukichangua chama bila kupingwa kwenye changuzi za serikali za mitaa pamoja na uchanguzi Mkuu kwa kuchaguliwa wabunge wote kutoka CCM pamoja na madiwani wa Kata zote.
Beda amesema kuwa kama mwenyekiti wa chama hicho
anawajibu wa kuwatetea wananchi walio kichangua chama kukaa madarakani na wala hana adhima ya kupinga kila jambo la
serikali ili mradi tu kama jambo jema na linamasirahi kwa umma yuko tayari
kulipongeza.
Alifafanua kuwa kuelekea miaka 44 CCM,kama chama
wanawajibu wa kuisimamia serikali katika utekelezaji wa ilani ya chama ambayo
ni mkataba kati yao na wananchi.
Aidha amejivunia mafanikio makubwa yaliyofanywa na CCM
katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kitaifa kama vile ujenzi wa reli wa
gari moshi ya umeme,ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha
lami,imalishaji wa shirika la ndege nchini,uimarishaji wa upatikanaji wa huduma
ya umeme vijijini na kuimarika kwa uchumi wa nchi kufikia wa ngazi ya kati.
Marry Anthony Mkazi wa Kijiji cha Milala Manispaa ya
Mpanda ambaye ni mwanachama wa CCM,alipongeza viongozi wa chama kwa kuweza
kufanya ziara hiyo ya upandaji miti pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi.
Aliongeza kuwa kama wanachama wanajivunia kuona chama
kina kuwa karibu zaidi na wananchi kwenye kuwatumikia kwa kuwa inaongeza
hamasa ya watu kuwa na imani kwa chama.