Askofu wa Jimbo la Mpanda Mkoa wa Katavi Eusebius Nzigilwa akiongoza ibaada maalumu ya maombezi ya aliyekuwa rais wa Tazania Dkt John Magufuli aliyefariki hivi karibuni,Ibaada hiyo imefanya katika kanisa la mtakatifu Maria Immaculata Mpanda Mjini Mkoa wa Katavi na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali.
Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda Askofu Eusebius Nzigilwa amewaomba watanzania kuomba Mungu Nchi ipate viongozi watakao msaidia Rais Samia Suluhu Hassan ambao hawata kuwa kwa manufaa yao binafsi na waadilifu na wachapakazi ili waweze kmsaidia kufanya kazi Rais Samia Suhulu Hassan.
Waumini wa Kanisa la Roman Catholic waliohudhuria katika ibaada ya kumuombea aliyekuwa rais wa Tanzania Dkt John Maguli aliyefariki hivi karibuni.Ibaada hiyo imefanyika mjini Mpanda Mkoa wa Katavi,.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda Askofu Eusebius Nzigilwa amewaomba watanzania kuomba Mungu Nchi ipate viongozi watakao msaidia Rais Samia Suluhu Hassan ambao hawata kuwa kwa manufaa yao binafsi na waadilifu na wachapakazi ili waweze kmsaidia kufanya kazi Rais Samia Suhulu Hassan.
Wito huu ameutowa wakati wa ibada ya kumwombea aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Magufuli iliyofanyika kwenye Parokia Kuu ya Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda parokia ya Maria Imakulata iliyohudhuriwa na Mapadri wa Jimbo lote la Mpanda na viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Katavi waliongozwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph.
Nzigilwa ameeleza kwenye mahubiri yake kuwa wapo baadhi ya watu huwa wanataka kuwa viongozi ili waongoze kwa manufaa yao binafsi.
Kanisa la Jimbo Kuu Mpanda la Mtakatifu Maria Immaculata Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Amesema Taifa baada ya kupitia kwenye changamoto hii watanzania wanaamini kuwa Taifa litaendelea kusimama kama lilivyokuwa .
Askofu Nzingilwa alieleza kuwa yeye kabla ya Rais Magufuli haja fariki Dunia wakati alipokuwa amelazwa Hospitalini alikuwa akiwasiliana na wasaidizi wa karibu wa hayati Magufuli kwani alikuwa akifahamiana nao .
Na katika mwasiliano yake na wasaidizi hao walimwambia kuwa hayati Magufuli wakati akiwa kitandani alipenda sana kuimba nyimbo za Dini za Kanisa la RC na alikuwa akiwashirikisha na wasaidizi wake kuimba nyimbo hizo .
Pia wamemweleza kuwa alikuwa akipenda sana muda wote kutembea na rozali akiwa ameiweka kwenye mfuko wake wa saruali na alikuwa haiachi hata siku moja na aliitumia zaidi kusali hasa pale ambapo alipokuwa na jambo linamtatiza .
Amesema siku moja kabla ya kifo chake aliwaomba wasaidizi wake wamwite KadrinaliPolikapo Pengo na Paroko wa Paroka ya Mtakatifu Peter Ositabeyi.
Askofu wa jimbo la Catholic Jimba la Mpanda Mkoa wa Katavi Eusebius Nzigilwa(nne kushoto)akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mpanda,Bi Jamila Yusuph (tatu kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na mapadri na viongozi wa serikali baada ya ibaada ya kumwombea aliyekuwa rais wa Tazania Dkt John Magufuli aliyefariki hivi karibuni.
Ameeleza kuwa Kadrinali Pengo na Paroko wa parokia hiyo waliweza kufika Hospitalini hapo na waliweza kuongea nae hayati Magufuli na siku iliyofuata alifariki Dunia .
Hari hiyo inaonyesha kuwa hayati Magufuli amekuwa katika imani na ndio maana aliongea na viongozi wa Dini kwa mara ya mwisho.
Amewaomba Wanzania kumwombea Rais Samia Sluu Hassan katika kipindi hiki cha majonzi aweze kupata Makamu wa Rais atakaeweza kumsaidia kufanya kazi .
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph alisema hakuna haja ya kuendelea kufadhaika na badala yake tuendelee kumwezi kwa kufanya kazi .
Amesema katika kipindi chake cha uongozi amefanya mambo makubwa kwa Mkoa wa Katavi kama vile ujenzi wa barabara za kiwango cha lami zinazounganisha Mkoa huu na Mikoa mingine, ujenzi wa vituo vya afya nane Hospiitali za Wilaya tatu na moja ya Rufaa ya Mkoa ,ujenzi wa bandari ya Karema, safari za ndege,ujenzi wa reli ya standa geji na miradi ya maji .
Monsinyori Padri George Kisapa ambae ni makamu wa Jimbo Katoliki la Mpanda alisema kuwa toka amekuwa Padri haja wahi kuona maendeleo yaliopatikana katika Mkoa wa Katavi na nchi kwa kipindi kifupi kama alivyofanya Rais Magufuli.