KATAVI KUANDAA KALENDA ZA LISHE KUPINGA UDUMAVU

Waziri wa Afya,Dkt Doroth Gwajima(kulia)akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Juma Homera(kulia) wakiwa pamoja kwenye ziara ya kikazi mkoa humo.

Na Zillper Joseph KTPC,Katavi.

Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dakta Dorothy Gwajima amewataka maafisa lishe wa mkoa na wilaya za mkoa wa Katavi kuandaa kalenda maalum zitakazokuwa zinafundisha namna ya kumlisha mtoto ili kuondokana na tatizo la udumavu.

Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dakta Dorothy Gwajima amewataka maafisa lishe wa mkoa na wilaya za mkoa wa Katavi kuandaa kalenda maalum zitakazokuwa zinafundisha namna ya kumlisha mtoto ili kuondokana na tatizo la udumavu

Dakta Gwajima ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kikazi mkoani hapa ambapo amesema kalenda hizo zitasaidia kuongeza uelewa kwa wananchi hasa waishio maeneo ya vijijini

‘Tengeneza kalenda lenye picha za vyakula vyote sambaza kwenye ofisi za kata, zahanati na maeneo mengine wakienda kuhudumiwa huko wanapata na elimu’. alisema Dk. Gwajima

Ameongeza kuwa kalenda hizo zitabeba orodha ya makundi ya vyakula kulingana na asili ya vyakula vinavyopatikana katika kila Halmashauri na itaje vyakula gani vinafaa kwa mlo wa asubuhi, mchana na jioni 

Akizungumzia changamoto hiyo mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera amesema tatizo kubwa ni uelewa duni wa wananchi wa namna ya kula mlo kamili wakati Katavi ina vyakula vya kutosha

‘Hii ni nchi ya asali na maziwa, tunaposema hivyo si kwamba tunajisifia bali ni kwa sababu vyakula vya aina yote vinastawi hapa. Tuna karanga, viazi, ufuta, mahindi, mchele, kunde, maharage, choroko, ni vyakula vingi kwa kweli’ alisema Homera.
Homera ameongeza kuwa licha ya kuwa na mifugo mingi maziwa yanayopatikana kutokana na mifugo hiyo yanaishia kwenye biashara huku familia ikiachwa bila maziwa ya kunywa

Amesema kuwa familia zilizo nyingi mkoani hapa zinatumia wali kama chakula kikuu bila kufuata mchanganyiko wa vyakula hali inayopelekea udumavu kwa watoto 

Akizungumzia tatizo la udumavu Mganga Mkuu wa mkoa wa Katavi Dk. Omari Sukari amesema mpaka mwaka 2020 asilimia 33 ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano waligundulika na tatizo la udumavu

 Dk. Sukari amesema watoto hao ni wale waliofikishwa katika zahanati na vituo vya afya ambapo walipata huduma ikiwemo ya kinamama kufundishwa jinsi ya kumlisha mtoto

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages