Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Mpanda.
Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi .
Wakazi wa Mkoa wa Katavi wametowa tamko la kupokea kwa mshituko mkubwa wa kifo cha Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa upande wa Wanakatavi ni Rais ambae ameacha alama kubwa na isiyofutika mioyoni mwa Wanakatavi kwa ujumla wanamkumbuka kwa ujasili wake ,uzalendo na upendo mkubwa alioonyesha ni mfano wa kuigwa na kama wanakatavi wanalodeni kubwa sana la kuenzi mazuri yote
Tamko hilo la wananchi wa Mkoa wa Katavi limetolewa kwa niaba yao na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera katika tamko lililotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamira Yusuph ambae aliagua kilio na kutokwa machozi wakati akisoma taarifa hiyo.
Amesema anaposema kuwa Rais John Magufuli aliwapenda wana Katavi lazima kuvuta kumbukumbu ya Katavi ya mwaka 2015 kabla ya kuingia madarakani na leo anapowaacha wakiwa 2021.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa mkoa huo,Dkt Omary Sukari
Mkoa huu umetengenezewa barabara za kiwango cha lami kutoka Mpanda kwenda Tabora ambapo ujenzi wake upo karibu kukamilika muda si mrefu , Mpanda kwenda Uvinza na Sumbawanga hadi Mpanda ambazo zinafanya kazi na kuwa kitovu cha uchumi wa Mikoa ya Rukwa , Kigoma na Tabora .
Pia uimarishaji wa safari za gari moshi ya Tabora hadi Mpanda Katavi pamoja na mpango wa ujenzi wa reli ya kisasa standard gage Mpanda kuelekea Karema ambayo ujenzi wake unaendelea na uwanzishwaji wa safari za ndege kwa waki mara na safari hizo za ndege alifungua yeye mwenyewe Rais Magufuli alipofanya ziara Mkoani Katavi mnamo tarehe 12 Oktoba 2019.
Aidha kwa kutambua kuwa Mkoa wa Katavi ni wenye uzalishaji mkubwa ameelekeza kuunganishwa na Grid ya Taifa na ujenzi wa miundo mbinu hiyo inakamilishwa oktoba 2021 sambamba na usambazaji wa umeme wa REA ambapo mwanga umewafikia wananchi kwa asilimia 90 hadi sasa.
Homera amesema watakuwa wachoyo wa fadhila kama wasipokumbuka alivyowajali wanyonge wa Katavi kama alivyosisitiza kuwa yeye ni Rais wa wanyonge kwa kuboresha huduma za jamii hasa katika Afya ,elimu na Maji wote watakuwa watakuwa mashahidi kuwa wamefaika na elimu ya msingi na Sekondari bila malipo ujenzi wa vituo vya afya katika Mkoa huo vinane vinavyotowa huduma kwa sasa na Hospitali nne za Wilaya na Hospitali moja ya Rufaa ya Mkoa.
Ameeleza hakika atakumbukwa sana hasa na akina mama ambao walikuwa wanakumbwa na adha ya upatikanaji wa maji katika familia zao na hata kupelekea ndoa kuvunjika .
Ametowa rai kwa wananchi wa wa Mkoa wa kuendelea kuwa watulivu wastahimivu na kuendelea kuimarisha upendo ,mshikamano ,undugu na umoja hasa katika kipindi hiki kigumu huku wakimwombea heri mbele za Mwenyezi Mungu apumzike kwa amani.
Ametowa rai kwa wananchi wa wa Mkoa wa kuendelea kuwa watulivu wastahimivu na kuendelea kuimarisha upendo ,mshikamano ,undugu na umoja hasa katika kipindi hiki kigumu huku wakimwombea heri mbele za Mwenyezi Mungu apumzike kwa amani.