KATAVI WAMPONGEZA DTK MPANGO.

 



Dkt Philip Mpango.

Na George Mwigulu KTPC,Katavi.

Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamempongeza Dkt Philip Mpango kwa kuteuliwa kuwa makamo wa rais wa Tazania huku wakiwa na imani kubwa dhidi yake kuwa atautumikia vyema.


Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamempongeza Dkt Philip Mpango kwa kuteuliwa kuwa makamo wa rais wa Tazania huku wakiwa na imani kubwa dhidi yake kuwa atautumikia vyema.

Uteuzi huo  umefanyika baada ya kufariki dunia kwa aliye kuwa rais wa Tazania Hayati Dkt John Magufuli na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa makamo wake Mh Samia Suluhu Hassain ambaye kwa sasa ndiye rais huku nafasi ya Makamu akimteua Dkt Mpango.

Pongenzi hizo wamezitoa leo kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao ambapo wameonesha kuwa na imani kubwa ya kuteuliwa Dkt Philip Mpango ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Mariam Hassan Mkazi wa Mtaa wa Nadukani Manispaa ya Mpanda anasema kuwa uteuzi humo umeshangazwa na watu wengi kutokana na kuwa Dkt Mpango hakuwa miongoni mwa watu ambao hawakutajwa kabisa midomoni mwa watu kuwa atashika wadhifa huo.

Ameeleza kuwa ni uwazi usiofichika kuwa uwezo,weledi na maadili ya Dkt Mpango sio ya kutiliwa shaka kwani kabla ya uteuzi huo akiwa waziri wa fedha na mipango ameonesha kazi nzuri ambao taifa kulifanya kufikia uchumi wa kati.

Anthony Shigela Mkazi wa Mtaa wa Misukumilo ameeleza kuwa kazi iliyofanywa na Dk Mpango kwenye wizara ya Fedha na Mipango ni kubwa zaidi,Hivyo ataendelea na kasi hiyo hiyo.

''...naimani kuwa anakwenda kuwa mshauri hondari wa rais Samia Suluhu Hassain,mambo ambayo yalikuwa bado kutekelezwa kabla ya kifo cha mpendwa wetu Magufuli yanakwenda kutekelezeka kwa kasi kubwa'' amesema Shigela.

Wande Mashalla ambaye ni mfanyabiashara katika soko kuu la Mpanda amemweleza Dkt Mpango kama kiongozi mwenye sifa zilizojitosheleza na mwenye uwezo wa kuhudumu nafasi nyeti kama hiyo.

Aidha amempogeza rais Samia Suluhu Hassain kwa kumteua Dkt Mpango kuwa Makamo wa rais kwani hajafanya makosa na kuwa shughuri za ujenzi wa taifa kwa maendeleo utazidi kuwa juu.


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages