MILA NA DESTURI KIKWAZO UTOAJI WA ELIMU YA UZAZI KWA VIJANA KATAVI.


Na George Mwigulu KTPC,Katavi.

Afya ya uzazi ni suala ambalo ni muhimu katika jamii yoyote,ambapo serikali kwa kutambua hilo,inafanya juhudi za kulinda wasichana na wanawake katika kupata huduma muhimu za afya ya uzazi.Afya ya uzazi ni suala ambalo ni muhimu katika    jamii yoyote,ambapo serikali kwa kutambua hilo,inafanya juhudi za kulinda wasichana na wanawake katika kupata huduma muhimu za afya ya uzazi.

Licha ya Juhudi hizo baadhi ya vijana wamejikuta wakipoteza mwelekeo wa maisha kutokana na kuikosa elimu ya afya ya uzazi kwa sababu ya mila na tamaduni zinaonekana kuwapa kibali thabiti wazazi,walezi pamoja na jamii nzima kutotoa  elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wao.

Kuificha elimu ya afya ya uzazi kwa vijana imeleta sura nyingine ya hatua ambayo baadhi ya vijana wamejikuta wakiingia kwenye mapenzi ambayo si salama,huku hatima ya elimu yao ikisalia mashakani na pengine kwa kushindwa kutimiza ndoto zao za kimaisha.  

Agelina Mashala mkazi wa kijiji cha Ilangu Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi anathibitisha kuwa hawezi kuwaambia vijana wake kuhusu  afya ya uzazi kama kutumia kondomu ama vidonge kwani atakuwa kama anawaelekeza katika hatua nyingine ya uzinzi kwenye maisha yao.

"…sisi ni waafrika hatujafundishwa na mababu zetu kuwaeleza watoto wetu mambo ya aibu namna hiyo,haitupasi hata kidogo masuala ya kitandani kuyaweka hadharani kwa watoto,naomba fahamu hivyo habari za maisha ya kizungu hayana maana kwetu" amesema Agelina.

Mitizamo kama hiyo  wasichana wengi inawafanya kutokujua haki zao au wahajui watafute wapi msaada isipokuwa kwenye famila zao au taasisi za kitamaduni ambazo zimegeuka na kuwafanya wahanga wa mimba na ndoa za utotoni.

Kwa maana hiyo  vijana wengi wamejengewa woga wa kutokutoa taarifa za kushawishiwa na kulazimishwa kufanya vitendo vya ngono  hata wakiwa na umri mdogo iwe kunyanyaswa kwenye ndoa kwa sababu hawana imani na mfumo wa kisheria pamoja na familia na jamii kwa ujumla.

Mzee wa kimila Shigera Funuki mkazi wa kijiji cha Mazwe wilaya ya Tanganyika mkoani  humo amesema suala la kutokubaliana na elimu ya afya ya uzazi inadhaniwa kuwa ni njia ya kuwalinda dhidi ya ngono  na mimba kabla ya ndoa.

Shigera anasema  ‘’ afya ya uzazi inawafanya wasichana kuwa na ufahamu mkubwa wa masuala ya kingono ambayo yanamfanya mtoto kutamani kufanya majaribio ya kujamiana na kupata mimba ambazo zinashusha heshima za familia na kushusha kiasi cha mahari  ambayo familia inayopokea’’.

Mkazi wa Kijiji cha Mishamo Wilaya ya Tanganyika Mariam Hussein ambaye mwanaye wa kike (jina limehifadhiwa) amepata ujauzito  akiwa na umri wa miaka 13 na kukatisha masomo yake amesema kuwa utendaji wa kitamaduni  unadhoofisha upatikanaji wa elimu ya afya ya uzazi na kutengeneza ukuta kati ya wazazi/walezi na watoto.

"sikuona umuhimu wa kumpatia elimu ya afya ya uzazi binti yangu  kutokana na jinsi alivyokuwa mtulivu na mpole mwenye kupenda elimu sana…nilishangaa ghafula kuona mabadiliko kwenye mwili wake na kuwa tayari  amepata mimba,nimejiidanganya mwenyewe na kumwangamiza mwanangu’’ amesema Mariam.

Jambo la kusitaajabu zaidi ni namna mbavyo wazazi/walezi wa kiume wamekaa mbali zaidi na suala la afya ya uzazi huku wakiwaachia majukumu hayo wanawake pekee huku kiza cha ni nani awajibike kikiwa bado hakifahamiki kutokana na ukandamizaji wa afya ya uzazi.

Kwa mujibu wa utafiti  afya ya uzazi na mtoto wa mwaka 2015/16,uliofanywa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee nna Watoto,Kwa Tazania umeonesha kuwa mkoa wa Katavi ndio mkoa unaongoza kwa mimba za utotoni  nchini.

Utafiti huo umeonesha kuwa 27% ya wasichana wa miaka 15-19 wameshaanza uzazi ,21% walikuwa wameshazaa mtoto hai mmoja na 6% walikuwa wajawazito wakati wa utafiti.

Mkoa wa Katavi 45% ya wasichana wa miaka 15-19 walikuwa wameshaanza  angalau uzazi ,33.3%  wakiwa wameshazaa angalau mtoto mmoja hai  na 11.8% walikuwa wajawazito wakati wa utafiti.

Kutokana na tafiti hizo Mkoa wa Katavi kwa kutambua  kuwa vijana katika jamii wanatajwa kuwa ni idadi kubwa ya watu katika jamii  lakini changamoto zinazowakabili  ni nyingi huku ikiwa ni kundi ambalo kwa kawaida wanahisi kutokueleweka katika jamii licha ya mahitaji yao maalumu.

Suala moja ambalo linakwamisha vijana ili kufikia uwezo wao kikamilifu wa maendeleo ya kielimu na uchumi nila afya ya uzazi,Serikali ya mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali inalishughurikia dhati suala ya afya ya uzazi.

Elida Machungwa Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Mkoa wa Katavi, wakati wa mdahalo unaohusu Afya ya Uzazi na Ukatili wa Kijinsia uliofanyika Manispaa ya Mpanda  amesema kuwa tatizo la mimba za utotoni ni changamoto ambayo inahitaji juhudi za pamoja kati ya serikali,wananchi na wadau wa maendeleo kutoa elimu kwa jamii.


‘’  elimu inapaswa kuzidi kutolewa kwa vijana pamoja na jamii kwa ujumla ili jamii iweze kubadili mitizamo hasi hasa ambayo inahusuiana ukatili dhidi ya watoto na kuwanyima haki yao ya kupata elimu ya afya ya uzazi’’ amesema Mratibu huyo.

Amefafanua kuwa  ni wakati sasa umefika kwa jamii mkoani humo kupinga kwa nguvu zote mimba na ndoa za utotoni kutokana na waathirika zaidi kuwa ni wasichana ambao hukatishwa masomo na kukosa fursa za kiuchumi kwa ajili ya maendeleo .

Afsa Vijana Manispaa ya Mpanda,Rozina Ngonyani amesema kuwa ili kuwawezesha wanafunzi na vijana kujielimisha mambo kuhusu afya ya uzazi .Serikali kwa kushirikiana na wadau wanapaswa kuandaa midahalo kupitia klabu zilizoanzishwa katka shule za msingi na sekondari.

"…vijana walio nje ya mfumo wa elimu ili kuhakikisha vijana wote wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu Afya ya Uzazi na kupinga ukatili  wa kijinsia na mimba za utotoni zinazosababishwa na ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi  ni muhimu kufanya mikutano mbalimbali ya kutoa elimu’’ Amesema Rozina.

Kwa upande wa mashirika ya siyo ya kiserikali (NGO) kwa mkoa wa Katavi Taasisi ya Hope Center Tazania ili kuendeleza mapambano dhidi ya kuwanyima haki vijana kupatiwa elimu ya afya ya uzazi wamefanikiwa kufanya semina na waaadhi wa habari ambao watakuwa mabaloza kwa kuelimisha afya ya uzazi.

Mkurugenzi Mtengaji wa Hope Center Tazania Halima Lila  akizungumza na wanahabari wakati akiendesha semina hiyo alifafanua kuwa wameamua kuishirikisha makundi ya jinsia zote katika utoaji wa elimu ya afya ya uzazi hasa kwa wanaume kwa sababu mara nyingi wanaume ndio wanaofanya maamuzi ndani ya familia zao.

Halima alieleza kuwa kunamatokeo makubwa hadi sasa yamepatikana baada ya kuwashirikisha wanaume katika masula ya elimu ya afya ya uzazi kwani wanaume wameonesha utayari mkubwa kupitia semina walizo toa kwao na kuwa mabalozi wa kutoa elimu kwa wengine.

Aidha amebainisha kuwepo kwa changamoto ya kuwafikia watu wenye ulemavu hasa wasichana kwani jamii bado inadhana potofu ya kuwaficha.Hivyo bado wanaendelea kuwatafuta popote pale walipo moani Katavi na kuwafikia  kuwapa elimu.


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages