NAIBU WAZIRI KUNDO;GHARAMA YA VIFURUSHI VYA MAWASILIANO VIMESHUKA

 

Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano ya Teknolojia na Habari Mhandisi Andrew Kundo

Na Mwandishi Wetu KTPC,Katavi.

Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano ya Teknolojia na Habari imepiga hatua kubwa ya kuboresha na kushusha zaidi gharama za huduma za mawasiliano  nchini kufikia kiwango cha juu cha Tshs 9.35 kwa MB1 ambazo ni nafuu zaidi. 


Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano ya Teknolojia na Habari imepiga hatua kubwa ya kuboresha na kushusha zaidi gharama za huduma za mawasiliano  nchini kufikia kiwango cha juu cha Tshs 9.35 kwa MB1 ambazo ni nafuu zaidi.

Gharama hizo ni nafuu ikilinganishwa na nchi ya Afika Kusini inayotoza Tshs 37 kwa MB1 huku baadhi ya nchi za Afrika mashariki na Kati kutoza gharama ya kufukia kiwango cha juu cha Tshs 12 hadi Tshs 15 kwa MB1

Naibu Waziri wa Mawasiliano ya Teknolojia na Habari  Mhadisi Andrew Kundo,amesema hayo kwenye ziara yake manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakati anaelezea namna ambavyo serikali imedhamilia kufanya huduma ya mawasiliano inayotengeneza fursa za kiuchumi.

Kundo amefafanua kuwa kabla ya wizara ya Mawasiliano ya Teknolojia na Habari kuanzishwa kuna baadhi ya makampuni ya simu yalikuwa yakitoza kufikia  gharama ya mawasiliano ya Tshs 40 kwa MB1.


Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano ya Teknolojia na Habari imepiga hatua kubwa ya kuboresha na kushusha zaidi gharama za huduma za mawasiliano  nchini kufikia kiwango cha juu cha Tshs 9.35 kwa MB1 ambazo ni nafuu zaidi.

Baadhi ya Kampuni za mawasiliano ya simu licha ya kusema vigezo na masharti kuzingatiwa lakini wananchi hawakuwa na uelewa ni namna gani vigenzo hivyo vinazingatiwa ambapo vilisababishwa na changamoto ya wananchi kuwa na mazoea ya kutumia huduma ya mawasiliano bila kujua ubora wake. 
Katika huduma za mawasiliano ya kiwango cha chini pamoja na kutegeneza mazingira bora ya uwekezaji katika huduma ya mawasiliano,Naibu Waziri huyo alisema kuwa kiwango cha chini kimewekwa kuhakikisha ubora wa huduma unatolewa na watoa huduma ni lazima uzingatie ubora wa viwango vilivyowekwa na mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) ambapo serikali itakapo tambua kunatatizo la kutokuwa na ubora wa huduma itatoa adhabu ya penati kwa kampuni husika.

Fedha zitakazopatikana kutokana na penati za kila baada ya mienzi mitatu zinazotokana na kuporomoka kwa ubora,Fedha hizo badala ya kuingizwa serikalini bali zitarudishwa kwenye kampuni ya simu ili kusaidia kutengeneza mpango wa uwekezaji kwenye maeneo ambayo serikali imegundua kuna viwango visivyo na ubora.

Alisema licha ya kuwa na vifurushi vya mawasiliano ya simu ya aina ya  kujinga vifurushi vya ukomo na visivyo na ukomo pamoja na salio la kawaida ambalo linakatwa taratibu kulingana na matumizi ya mtumiaji  vyote hivyo gharama yake imeshushwa zaidi.

‘…kuna changamoto ya watumiaji wa vifurushi vya ukomo,kwa kutambua hilo ndugu zangu kama kitakuwa kinaelekea ukomo wake kufika mtumiaji atakuwa na uwezo wa kukihamisha kwa mtumiaji mwingine,Pia kwa mtumiaji ambaye MB zake zimekishwa bila yeye kufahamu wakati anatumia huduma ya mawasiliano ya internet na kama anasalio la kawaida,Ni wazi atambue kuwa salio lake hilo halitatumika hadi kwa yeye mwenyewe kuruhusu” alisema Kundo. 
Katika hatua nyingine Naibu waziri huyo amesema kuwa makampuni ya simu bado hayajafikia kiwango cha kutoa huduma kwa kiwango cha 4G katika baadhi ya maeneo,Hivyo serikali haitakuwa na pingamizi kuingia kwenye mfumo wa 5G kama yatakuwa yamekuidhi vigezo katika utoaji wa huduma kwenye maeneo yote kwa kiwango cha 4G.

Aidha amewaomba wananchi kuendelea na matumizi mazuri ya njia mbalimbali za mawasiliano kwa kutokujihusisha na usabazaji wa habari za uwongo na udhalilishaji kwa watu au serikali sambamba na kuwafichua waharifu wa njia ya mitandao.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages