WANANCHI KATAVI WANUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI SAFI.

 

Na Mwandishi Wetu KTPC,Mpimbwe.

Huduma ya maji inayotolewa na wakala wa usambazaji  maji na usafi wa mazingira (RUWASA) Mkoa wa Katavi imewafikiwa kuwahudumia wananchi wa mkoa huo maji safi na salama kwa asilimia 70  ambapo wanufaika zaidi ya laki nne katika mkoa wa katavi wapata huduma ya maji safi na salama.

HHuduma ya maji inayotolewa na wakala wa usambazaji  maji na usafi wa mazingira (RUWASA) Mkoa wa Katavi imewafikiwa kuwahudumia wananchi wa mkoa huo maji safi na salama kwa asilimia 70  ambapo wanufaika zaidi ya laki nne katika mkoa wa katavi wapata huduma ya maji safi na salama.

ayo yameelezwa na meneja wa RUWASA mkoa wa katavi Mhadisi,Peter Ngunula katika taarifa aliyoisoma mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Jamila Yusuph kwenye uzinduzi wa wiki ya maji uliofanyika kata ya majimoto halmashauri ya mpimbwe wilaya ya mlele.

Mhadisi Ngunula amesema kuwa huduma ya maji imeendelea kuimarika kwa kusogeza vituo vya maji 1619 kwa mkoa wa katavi huku akieleza changamoto ambazo ni pamoja na vitendea kazi,watumishi pamoja na ofisi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi huo Athony Malale Mkazi wa Kijiji cha Majimoto ameishukuru serikali kupitia wakala wa usambazaji  maji na usafi wa mazingira kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo.

Ameeleza kuwa hapo awali walipata shinda kubwa ya kukosa maji safi,hali iyosababisha kutarisha afya zao kwa kutumia maji kutoka vyanzo ambavyo sio salama.

Aisha Hussein amebainisha kuwa kwa sasa ndoa zao ziko salama kutokana na ukaribu wa maji yanapopatikana kwani hapo mwanzo walikuwa wakiyafuata kwa ubali mrefu zaidi jambo ambalo liliwafanya kuchelewa kurudia nyumbani.




Aisha am.eweka wazi kuwa kutokana kuletewa maji karibu na makazi yao wako tayari kutunza miundombinu yote ya maji kwa kutumia mfumo wa ulizi shirikishi ili kuwabaini wote wenye nia mbaya ya kufanya uharibifu wa mabomba ya maji.

Mkuu wa wilaya ya mpanda Jamila Yusuph  akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa katavi Juma Zuberi Homera amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji.

Wiki ya maji ambayo huadhimishwa mwenzi March kila mwaka  imebebwa na kauli mbiu isemayo THAMANI YA MAJI KWA UHAI NA MAENDELEO.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages