Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi,Christopher Nakua
Na Walter Mguluchuma Katavi
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Takukuru Mkoa wa Katavi wamemkamata katibu wa Kitongoji cha Magula Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Egid Damas Ntila maarufu kwa jina la mwalimu Egid Peter kwa kosa la kuomba rushwa ya shilingi laki tatu kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Takukuru Mkoa wa Katavi wamemkamata katibu wa Kitongoji cha Magula Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Egid Damas Ntila maarufu kwa jina la mwalimu Egid Peter kwa kosa la kuomba rushwa ya shilingi laki tatu kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Cristopher Nakua aliwaambia wandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na Takukuru hapo machi 11 huko katika kitongoji cha Magula Kata ya Sitalike.
Katika tukio hilo mtuhumiwa Egid Ntila ambae ni Kaimu Katibu Katibu wa Serikali ya Kitongoji cha Magula kilichopo katika Kijiji cha Mtisi Kata ya Sitalike Wilaya ya Mpanda alipokea Rushwa ya fedha kiasi cha shilingi elfu Hamsini ikiwa ni sehemu ya shilingi laki tatu ambazo alikuwa ameziomba kutoka kwa mlalamikaji jina limehifadhiwa .
Nakua ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo aliomba Rushwa hiyo ya fedha ili amuuzie mlalamikaji eneo la kufanyia biashara katika soko jipya lililoko kwenye kitongoji hicho ambapo viwanja vilikuwa vikitolewa kwa ajiri ya watu kufanyia biashara hapo .
Amesema kuwa utaratibu wa kutowa viwanja vya kufanyiia biashara hapo vilikuwa vikitolewa bure kwa wale ambao walikuwa wamewahi kuomba hata hivyo Katibu huyo hakufanya hivyo na badala yake alimtaka mlalamikaji ampatie kasi cha shilingi laki tatu kama rushwa ndio aweze kumpatia eneo kwenye soko hilo
Amesema baada ya mtuhumiwa kuomba Rushwa hiyo kutoka kwa mlalamikaji Takukuru walipata taarifa hizo na ndipo walipo andaa mtego na kufanikiwa kumkamata mtuhimiwa huyo akipokea kiasi cha Tshs 50 000 katia ya shilingi laki tatu .
Takukuru Mkoa wa Katavi wanaendelea na uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili huyo na pindi utakapokuwa umekamilika na kuthibitika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani ili akajibu tuhuma zinazo mkabili .
Katika hatua nyingine Takukuru Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya Mashitaka Mkoani Katavi imefanikiwa kufungua kesi mbili Mahakamani za makosa ya Rushwa .
Nakua alizitaja kesi hizo ni kesi ya kwa inawahusu Pridance Anacredo pamoja na Varanto Wiliamu ambao walikuwa ni viongozi wa Amcos Mishamo
Amesema watu hao wameshitakiwa kwa tuhuma za kufanya kosa la kutumia matumiz yai madaraka yao vibaya kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na 11 ya mwaka 2007 wameshitakiwa kwa huhuma za kujipatia jumla ya shilingi milioni nne kama mkopo isivyo halali na kesi hiyo imefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda .
Kesi ya pili ameitaja kuwa ni inayomkabili Juma Mnyongalule ambayo imefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Katavi ambapo mtuhumiwa ameshitakiwa kwa kujipatia kiasi cha Tshs 3,750,000 isivyo halali.
Amesema mtuhumiwa huyo aliendelea kulipwa na kupokea fedha za mshahara kutoka Shirika la Reli Tanzania alikokuwa akifanyia kazi kama fundi Mchundo maarufu Pigilia wakati huo akiwa sio mwajiriwa tena wa shirika la Reli Tanzania kwa mujibu wa sheria