TANROAD YA IMARISHA BARABARA ZA LAMI KATAVI KUTOKA KM 1.9 HADI ZAIDI YA KM 235.



Meneja wawakala wa barabara nchini(TANROAD) Mkoa wa Katavi,Mhadisi Martin Mwakabende.


Na George Mwigulu KTPC,Katavi.


Zaidi ya Kilometa 235.68 za urefu wa barabara kuu zimefanikiwa kujengwa kwa kiwango cha lami Mkoa wa Katavi ikiwa ni hatua kubwa ikilinganishwa na kilometa 1.9 pekee zilizokuwepo tangu mkoa huo kuanzishwa.

Zaidi ya Kilometa 235.68 za urefu wa barabara kuu zimefanikiwa kujengwa kwa kiwango cha lami Mkoa wa Katavi ikiwa ni hatua kubwa ikilinganishwa na kilometa 1.9 pekee zilizokuwepo tangu mkoa huo kuanzishwa.

Mhadisi,Martin Mwakabende ambaye ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) Mkoa wa Katavi amebainisha hayo jana ofisini kwake alipokuwa akielezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya uchanguzi mkuu wa mwaka 2020.

Amebainisha kazi ya mradi wa ujenzi na uboreshaji wa barabara za kiwango cha lami inafanywa kujengwa kwa haraka sana kwa kipindi cha miaka nane ambapo ongezeko limekuwa kubwa la barabara za lami.

Ongezeko hilo la barabara za lami linasaidia ukuaji wa uchumi kwa wananchi wa mkoa huo kwa kuwa na uwezo wa kusafirisha bidhaa na mali zingine bila vikwazo na kurahisha usafiri kwa watalii wanaokwenda katika hifadhi ya taifa ya Katavi (KANAPA).


Urefu wa barabara za lami amesema utakuwa ukiongezeka kila mwaka wakati huo huo urefu wa barabara za changarawe ukipungua,Hii ni kwa sababu ya juhudi zinazofanywa na serikali kuendelea kujenga kwa lami barabara kuu na barabara za mkoa zenye kipaumbele zaidi.

Meneja huya amesema kuwa kunaujenzi na ukarabati wa viwango vya lami katika barabara mbalimbali mkoani Katavi zinazoingia na kutoka ndani ya mkoa.Na moja ni ujenzi mkubwa wa barabara kutoka Tabora-Ipole-Koga hadi Mpanda wenye kilometa 321.389 unaogharamiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa pamoja na Serikali Kuu.

''ujenzi wa barabara ya Tabora-Mpanda imejengwa kwa vipande vitatu kwa kiasi cha gharama ya fedha bilion 432 huku barabara hiyo ikiwa imekamilika kwa kiwango cha lami ni Km 222 huku daraja la Koga likigharimu Bilion 4.4'' alisema Mhadisi Mwakabende.






Amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2020/21 ukarabati wa barabara kuu za changarawe zenye urefu wa Km 343.20 zinazofanyiwa matengenezo ni barabara za Lyamba Lya Mfipa-Mpanda-Uvinza na Mpanda-Koga pamoja na ukarabati wa barabara za mkoa za changarawe zenye urefu wa Km 778.50

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuacha kufanya uharibifu wa alama za usalama barabarani unaofanywa na wakazi wanaoishi kandokando na barabara ya Sitalike-Mpanda.

Kwa upande wa wanachi wa Manispaa ya Mpanda,Alex Mwandu Mkazi wa mtaa wa Ilembo licha ya kuishukuru serikali kwa ujenzi wa miradi ya barabara kwa kiwango cha lami wameiomba serikali kuzidi kuimarisha miundombinu ya barabara.

Mwandu amesema kama barabara zitaimarika zitatoa mchango mkubwa kwenye sera ya uwekezaji kwa mkoa wa Katavi.






Mwajuma Ali Mkazi wa kijiji cha Stalike Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi alisema kuwa kwa sasa wanauwezo wa kusafirisha mazao yao ya biashara kwenda sokoni bila shida yoyote.

Ameeleza kuwa barabara zilizojengwa zimechangia kwa kiasi kikubwa watoto wao kwenda shule na kupunguza utolo shuleni uliokuwa ukisababishwa na ubovu wa miundombinu ya barabara.







 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages