BANGO MOJA DED AU DC KUTIMULIWA KAZI.


Na George Mwigulu KTPC

RAIS Samia Suluhu Hassain amewataka wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Wilaya kutatua changamoto za wananchi kutokana na uwepo wa mabago ya malalamiko na kero zilizopo katika maeneo yao yanayoandikwa wakati viongozi wakuu wakiwa ziarani lasivyo atawaondoa kazini.

Rais Samia amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na manaibu katibu wakuu.

Ameeleza kuwa ni kawaida ya baadhi ya viongozi wakifanya ziara mikoani na wilayani wanapokewa na mabango ya wananchi wakilalamikia kero mbalimbali ambapo masuala yanayolalamikiwa sio ya kitaifa. 

"Kwa sababu najua tunapokuja watu wanakuja na mabango mbio mnakwenda kuyakusanya na kuwanyuka watu kuwapelekea mnapokujua nyie ili wasiseme yao yanayowasibu,naomba kero za wananchi zishughurikiwe ,tunapokuja na kukuta bango moja mkuu wa wilaya au mkurugenzi umekwenda na tukikuta malalamiko kwamba mnawafinya wananchi wasiseme hivyo hivyo tutashughulikiana.

Nao baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamempogeza rais Samia kwa kuwafahamisha mapema watumishi wa umma kwani ni wazi bado kunachangamoto kubwa za kero ambazo bado hazijatatuliwa.

Anthony Mabula mkazi wa mtaa wa Makanyagio amesema kuwa kuna baadhi ya watendaji wa serikali kwa ngazi za wilaya wamekuwa wazembe kutatua kero za wananchi kitendo ambavyo kumekuwa na mrudikano wa kero.

"Kama kero zitatuliwa kwa wakati kama vile migogoro ya ardhi iliyopo na migogoro mingine,ndugu mwandishi na kuhakikishia kuwa jamii itakuwa na ustawi mzuri zaidi wa maendeleo"amesema Mabula.

Mariamu Abdalah amesema kuwa uongozi wa rais Samia hadi sasa umeonesha matumaini makubwa kuwa nchi inakwenda kwenye mabadiliko makubwa hasa ya watu kuwa wenye furaha.

Ameeleza kuwa viongozi wa serikali kwa ngazi zote wanapaswa kuwa weledi katika utendaji wa kazi zao za kuwatumikia wananchi wote sambamba na kutekeleza maagizo yake ya kutatua kero zote za wananchi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages