DC ATOA MWEZI MMOJA KITUO CHA AFYA KUANZA KUFANYA UPASUAJI

 



Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema kushoto akizungumza na wajumbe wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Madaba(hawapo pichani)katika kikao cha Baraza la madiwani kilichofanyika jana,ambapo ameagiza kituo cha Afya Mtyangimbole kata ya Mtyangimbole kuanza kutoa huduma ya upasuaji ili kuwasaidia wananchi hususani akina mama wajawazito wanaohitaji huduma hiyo,katikati Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Shafi Mpenda na kulia mwenyekiti wa Halmashauri Theofenes Mlellwa,


Na Muhidin Amri KTPC,Songea

MKUU wa wilaya ya Songea Pololet Mgema,ametoa mwezi mmoja kwa  Halmashauri ya wilaya Madaba kuhakikisha kituo cha Afya Mtyangimbole kinatoa huduma ya upasuaji ili kuwaondolea kero wajawazito kwenda  Songea mjini umbali wa km 125 kufuata huduma ya upasuaji. 

MKUU wa wilaya ya Songea Pololet Mgema,ametoa mwezi mmoja kwa  Halmashauri ya wilaya Madaba kuhakikisha kituo cha Afya Mtyangimbole kinatoa huduma ya upasuaji ili kuwaondolea kero wajawazito kwenda  Songea mjini umbali wa km 125 kufuata huduma ya upasuaji.

Mgema ametoa agizo hilo jana, wakati akitoa salamu za Serikali katika kikao cha robo ya tatu cha Baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.


Alisema,hajaridhishwa kuona  akina mama wanaohitaji huduma ya upasuaji bado wanalazimika kwenda makao  makuu ya wilaya  Songea mjini umbali wa km 125 kufuata huduma ya upasuaji.


Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya, Serikali imekamilisha ujenzi wa kituo cha Afya Mtyangimbole  tangu mwaka jana kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za afya kwa wakazi wa kata hiyo na maeneo  ya jirani.

“pamoja na kazi nzuri ambayo Halmashauri mnaifanya, lakini haipendezi kusikia ving’ola vya gari la wagonjwa la kituo cha Afya Madaba linapeleka mama mjamzito Songea kwa ajili ya upasuaji,nakuomba sana Mkurugenzi na Timu yako anzeni kutoa huduma ya upasuaji katika kituo cha Mtyangimbole”alisema.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Mpenda alisema, ujenzi wa kituo cha Afya Mtyangimbole ulikamailika mwaka uliopita,hata hivyo changamoto kubwa ni uhaba wa watumishi katika Halmashauri hiyo.

Alisema,katika kituo cha Afya Mtyangimbole kuna Daktari mmoja ambaye  kimsingi kutokana na ukubwa wa kituo hicho hatoshi kutoa huduma kwa wananchi wote.

Hata hivyo alisema,wanachofanya ni wahudumu kutoka maeneo mengine hususani  waliopo katika kituo cha Afya Madaba kwenda Mtyangimbole na kuungana na mtaalam aliyekuwepo kutoa huduma kwa wananchi.

Alisema,serikali itakapo ajiri watumishi wa Afya kipaumbele cha kwanza ni kituo cha Afya Mtyangimbole  ili kwenda kuwahudumia wananchi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages