
Balozi wa Sweden aliyepo Nchini Tanzania,Mh Balozi Anders Sjoberg
Na George Mwigulu KTPC,Katavi.
Balozi wa Sweden Nchini Tanzania,Anders Sjoberg kupitia vyombo vya habari ametoa ujumbe kwa Chama Cha Waadishi wa Habari Mkoa wa Katavi (KTPC) kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Mei.3.

Katika maadhimisho hayo Balozi Anders amesisitiza licha ya kuwa nchi ya Sweden leo inafuraha ya kuwepo kusherekea uhuru wa habari na kujieleza,Sweden na Tanzania wamekuwa ni marafiki wa siku nyingi na wote wanatambua kwamba ni nguzo.Ikiwa sambamba na haki ya kupata taarifa ni muhimu kwa jamii inayoheshimu demokrasia na haki za binadamu.
Amesema kuwa nchi ya Sweden inaamini kwamba maendeleo ya nchi yoyote ile yanapatikana kwakupeana taarifa,kujadiliana kwa uwazi na kuwajibishana,Hivyo wataendelea kuungana na watanzania wote katika jitihada za kukuza na kuendeleza uhuru wa habari na kujieleza nchini.

Waadishi wa Habari Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari yaliyofanyika leo Mei 3,2021.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waadishi wa Habari Mkoa wa Walter Mguluchuma akifungua maadhimisho hayo leo katika ukumbi wa Kanisa Katoli Jimbo la Mpanda,amesema kuwa siku ya uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kwa wanahabari wote wa mkoa wa Katavi hivyo inawapasa kujikumbusha juu kuzingatia maadili ya uandishi wa habari wakati wa kuhabarisha uuma.
Mguluchuma amewataka waadishi wa habari kudumisha umoja na ushirikiano miongoni mwao kwa ajili ya kuhakikisha tanisia ya habari inaheshimika.

Mwenyekiti wa Chama Cha waadishi wa Habari Mkoa wa Katav,Walter Mguluchuma.
Amesema Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Dunia mwaka huu yana kauli mbiu ya HABARI KWA MANUFAA YA UMMA yanapaswa kuendana na jamii kuona umihimu zaidi wa vyombo vya habari katika kuchochea maendeleo nchini,Hivyo jamii inapaswa kuwalinda wanahabari wote.
Kwa niamba ya Katibu wa Chama Cha waadishi wa Habari Mkoa wa Katavi,Paschal Katona akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumury,Irene Temu amesema kuwa licha ya mafanikio ambayo imeyapata KTPC lakini bado wanahabari wanakabiliwa na changamoto nyingi.

Irene Temu Mwandishi Habari wa Uhuru Media Group Mkoa wa Katavi akisoma risala kwa niamba ya Katibu wa Chama hicho kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani.
Changamoto hizo ni pamoja na kuendelea kwa vitedo vya waadishi wa habari,kukamatwa,kupigwa,kuvunjiwa vifaa vya kutendea kazi ikiwa pamoja na kutishwa vikali na baadhi ya watu wasio na nia njema kwa wandishi wa habari nchini.
Irene Temu ameweka wazi kuwa changamoto zingine ni pamoja na ofisi ya KTPC kukosa ofisi kwa muda mrefu huku wakipanga kwenye nyumba za watu binafsi pamoja na kosefu wa usafiri.

Baadhi ya wadau wa habari waliohudhuria kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari yaliyofanyika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Haidary Sumury amewaomba waandishi kuendelea kutumia taalumu zao kwa ajili ya manufaa ya jamii husika kutokana na habari zao.
Aidha waandishi wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za habari ili kuondokana na mkanganyiko wa sitofahamu unaoweza kujitokeza pindi wanapotoa taarifa kwenye jamii kupitia vuombo vya habari wanavyo tolea taarifa.
Meya huyo katika hatua ya kukabiliana na changamoto ya kutokuwepo na umiliki wa ofisi ya KTPC na kuondokana na kupanga kwenye nyumba za watu binafsi,Ameweza kutoa eneo la uwanha kwa ajili ya kama hatua za awali za kuhakikisha inajengwa ofisi ya chama hicho.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi ,Haidary Sumury ambaye ni mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani.
Katika kuendelea na kutatua changamoto hiyo,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tannganyika,Hamadi Mapengo ametoa ofisi ya KTPC katika moja ya majengo ya yalipokuwa makao makuu ya halmashauri hiyo hapa Manispaa ya Mpanda kwa ajili ya kuepuka kupanga mitaani.

Kiongozi wa wa Dhehebu New Hevest Church,Askofu Mkuu Labani Ndimbenya.
Vilevile viongozi wa Dini waliohudhuria maadhimisho hayo wamesema kuwa waadishi wa habari ni koo katika jamii na hivyo wameombwa kuwa chachu ya kuibua changamoto kwa ajili ya maendeleo ya watanzania wote kiujumla.
Hata hivyo kwenye maadhimisho hayo Chama Cha waadishi wa habari kiliandaa mafunzo maalumu kutoka Taasisi ya Kupamba na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi pamoja na SIDO yenye lengo la kuwajengea uwezo wanahabari wa ufanisi katika kutimiza majumu yao ya kazi.
Pia KTPC wameweza kutoa vyeti ya kutambua ushirikiano kutoka baadhi ya Taasisi za umma na binafsi,ambapo katika kutambua mchango wao wametoa cheti kwa Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Katavi,Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya wilaya ya Tangantika,Mbunge wa Jimbo la Mpanda,Sebastian Kapufi,Ofsi ya Katibu Tawala na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.