IMAMU WA MSIKITI MPANDA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUFUNJA KAMERA YA MWANAHABARI.




Imamu wa Msikiti wa Makanyagio Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Mussa Hamisi (35) akiwa amejificha uso akiwa kwenye mahakama ya mwanzo ya mijini mapanda.

Na Mwandishi Wetu KTPC,Katavi.

Imamu wa Msikiti wa Mtaa wa Makanyagio Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Mussa Hamisi (35) mkazi wa mtaa wa Kawajese amefikishwa kizimbani katika mahakama ya Mwanzo ya Mpanda mjini kwa tuhuma za kufanya kosa la mshambulia mwandishi wa Channel Ten Mkoani humo,Paschal Katano na kumvunjia kamera yake kwa makusudi wakati akitekeleza majukumu ya kazi alipokuwa na mwandishi mwenzake wa ITV,Zilper Joseph.

Imamu wa Msikiti wa Mtaa wa Makanyagio Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Mussa Hamisi (35) mkazi wa mtaa wa Kawajese amefikishwa kizimbani katika mahakama ya Mwanzo ya Mpanda mjini kwa tuhuma za kufanya kosa la mshambulia mwandishi wa Channel Ten Mkoani humo,Paschal Katona na kumvunjia kamera yake kwa makusudi wakati akitekeleza majukumu ya kazi alipokuwa na mwandishi mwenzake wa ITV,Zilper Joseph.

Imamu huyo amefikishwa katika Mahakama hiyo hapo leo na kusomewa shitaka la kutenda kosa la Jinai la kuharibu mali kinyume na kifungu cha sheria 326 kifungu kidogo cha 1  cha kanuni ya adhabu mbele ya Akimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo ya Mpanda mjini Khadija Mtunguja.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo mnamo wa saa kumi na mbili jioni tarehe 14/04/2021 huko  katika eneo la msikiti wa Makanyagio Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

Siku ya tukio mtuhumiwa Mussa Hamisi alimvunjia kwa makusudi kamera ya mwandishi wakati wa ugomvu uliokuwepo baina ya waumini wa dhehebu la Waislamu wa pande mbili zilizo kuwa zikipingana  kwa kumkataa Imamu,Mussa Hamisi kuwa Imamu wa Msikiti huo hali iliyopelekea ugomvi huo kutokea na ndipo mwandishi huyo wa habari alipofanya kazi ya kutimiza wajibu wake.

Wakati mwandishi wa Habari akiendelea kutimiza majukumu yake ya kazi Imamu huyo alitoka ndani ya Msikiti na  kumvamia na kunyang'anya kamera yake na kuivunja kwa makusudi kwa kutumia goti na kuivunja vipandevipande.

Mtuhumiwa huyo baada ya kusomewa jina lake alikana kwa kusema sio jina lake ,alipoulizwa kwa mara ya pili alilikubali jina lilelile alilokuwa amelikana.Baada ya kuwa amelikubali jina hilo alilolikana mara ya kwanza,Hakimu alimuuliza mtuhumiwa kutenda kosa hilo na mtuhumiwa alikana kutenda.

Akimu Khadija Mtunguja aliahirisha kesi hiyo hadi April 28 mwaka huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa.Mtuhumiwa Imamu Mussa Khamisi amekwepa kwenda rumande baada ya kutimiza masharti ya mzamana ya  kiasi cha fedha laki nane.

Katika hatua nyingi mara baada ya kesi kuashirishwa,Nje ya Mahakama Katibu wa Baraza la Kislamu(BAKWA) Mkoa wa Katavi Omary Muna alitaka kuwazuia waandishi wa habari wasiweze kutimiza wajibu wao wa kupiga picha Mahakamani hapo wakati mtuhumiwa akitoka ndani ya mahakama.

Hata hivyo waadishi hao waliweza kutimiza wajibu wao kwa kufanikiwa kumpiga picha mtuhumiwa Imamu Mussa Hamisi ingawa  muda mwingi aliutumia kujificha usoni.


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages