LIGI YA LUPEMBE CUP YAZINDULIWA NSIMBO.




Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi Anna Lupembe.


Na George Mwigulu KTPC,Nsimbo.

Mbunge wa jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe ameonesha nia yake ya kuendelea kukuza vipaji vya vijana kupitia sekta ya michenzo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu kwa kuanzisha ligi itakayojumuisha timu 131 kutoka Kata 12 za jimbo lake.

Mbunge wa jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe ameonesha nia yake ya kuendelea kukuza vipaji vya vijana kupitia sekta ya michenzo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu kwa kuanzisha ligi itakayojumuisha timu 131 kutoka Kata 12 za jimbo lake.

Nia ya mbunge  huyo imeonekana hapo jana katika kata ya Katumba Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wakati wa uzinduzi wa ligi ya mpira wa miguu inayoitwa kwa jina la Lupembe Cup. 



Mgeni rasmi,Beda Katani Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Katavi akikagua timu kabla ya mchezo kuanza wa ufunguzi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya Mnyaki,Mbunge Anna Lupembe amesema kuwa ameanzisha ligi hiyo kama sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi ambayo inawahimiza wabunge kuendeleza michezo.


"  tunajua kuwa michezo ni ajira,michezo ni furaha na michezo ni amani na mimi kama mbunge wa jimbo la Nsimbo nimeamua nianzishe ligi ili niweze kuibua vipaji mbalimbali ndani ya jimbo la Nsimbo " amesema Anna Lupembe. 


Timu ga Mnyaki Fc kutoka Kata ya Katumba.

Amesema licha ya kuwa na lengo kubwa la kuibua vipaji vya vijana hao watakwenda katika maeneo mbalimbali kushiriki michenzo kwenye ngazi za juu zaidi,Hivyo wataweza kupata ajira na kukuza uchumi wao.


Mbunge huo ameweka wazi zawadi mbalimbali kuanzia mshidi wa kwanza wa mashindano hayo ambaye atajipatia kitita cha fedha cha Tsh 500,000/=,Mshindi wa pili Tsh 300,000/=,Mshindi wa tatu Tsh 200,000/=,Mshindi wa nne Tsh 100,000/= ,Mshindi wa tano Tsh 100,000/= pamoja na wachezaji bora wa ligi watapata zawadi. 


Timu ya Kiboko Rengers kutoka kata ya Sitalike.

" baada ya kukamilika ligi hii hatua itakayofuata ni kuanzisha ligi itakayojumuisha mabingwa wa kila tarafa za jimbo la Nsimbo ili kuweza kumpata bingwa mmoja wa jimbo lote atakaye pata zawadi ya Tsh 1,000,000/=,Mshidi wa pili atapata Tsh 700,000/=,Mshidi wa tatu atapata Tsh 500,000/=" amesisitiza Anna.



Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani akifungua ligi ya Lupembe Cup amempongeza mbunge huyo kwa nia yake jema ya kukuza vipaji kwa vijana.

Beda amesema kuwa mbunge huyo anapaswa kuingwa na wabunge wengine kuanzisha michezo kwani kufanya hivyo ni kushiriki kutekeleza ilani ya chama iliyoelekeza kukuza sekta ya michenzo.



Mashabiki wa mpira wa miguu waliojitokeza uwanjani.

Aidha katika mchenzo wa uzinduzi uliofanyika kwenye uwanja wa Mnyaki Kata ya Katumba ulizikutanisha timu za Kiboko Regers ya Kata ya Sitalike dhidi ya wenyenye wa mchezo huo Mnyaki Fc,ambapo baada ya mchezo kukamilika Mnyaki Fc walibuka washidi kwa kufunga goli 3 kwa 0 dhidi ya Kiboko Regers.


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages