MIZENGO PINDA AMEOMBA OMBI JINGINE KWA WATANZANIA.




Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda.


Na  Walter  Mguluchuma KTPC,Katavi 

Waziri Mkuu Mstaafu  Mizengo Pinda amewaomba watanzania waendelee kumwomba Mungu kwa kuwavusha salama katika kipindi kigumu ambacho kilikuwa akija wahi kutokea hapa  Nchini cha kuondokewa na Rais ambae alikuwa bado yupo madarakani akiwa haja maliza muda wake wa uongozi . 


Waziri Mkuu Mstaafu  Mizengo Pinda amewaomba watanzania waendelee kumwomba Mungu kwa kuwavusha salama katika kipindi kigumu ambacho kilikuwa akija wahi kutokea hapa  Nchini cha kuondokewa na Rais ambae alikuwa bado yupo madarakani akiwa haja maliza muda wake wa uongozi 

 Pinda alitowa ombihilo kwa Wanzania wakati alipokuwa akiwahubia waumini wa Kanisa katoliki kwenye Kanisa Kuu la Jimbo la  Mpanda Parokia ya Maria Imakulata  wakati wa ibada ya juma pili kwenye  ibada  ya misa  ya pili iliyoongozwa  na Padri  Filbert Baligwa ambae    pia ni mwasibu wa  Jimbo la Mpanda .

Alisema  Wanzania  waendelee kumwomba Mungu  kwa kuwawezesha kuvuka salama katika kipindi kigumu cha kuondokewa kwa ( kifo )cha  aliyekuwa Rais wa Tanzania John Magufuli wakati akiwa bado madarakani .

Amebainisha kuwa  ilikuwa haija wahi kutokea katika nchi hii kuondokewa na Rais ambae bado alikuwa kwenye kipindi cha uongozi  tulikuwa tunaondokewa na Marais waliyo maliza muda wao ``Alisema Pinda 

Alisema kuwa tuendelee kumwombea kwa Mungu kwani wakati wa maisha yake hayati  Magufuli alikuwa na hofu ya Mungu na ndio maana kila   mara alikuwa na hofu ya Mungu .

Pinda alieleza kuwa  ni jambo la kushukuru kwa Nchi ya Tanzania kumpata Rais Mama Samia Hassn  Suluhu  ambae walikuwa wakipanga mipango pamoja na Hayati Magufuli .

 Yeye anaamini kuwa yale yote yalikuwa yamepangwa kufanyika kwenye nchi hii wakati wa uongozi wa hayati Magufuli yataendelea kutekelezwa pasipo shaka yeyote

 Hivyo ni vema Wanzania wakampa ushirikiano mkubwa Rais  Samia Hassn Suluhu ambae ameanza vizuri kuongoza nchi yetu.

 Alisema kuwa wapo baadhi ya watu walikuwa na mashaka na kuongozwa na Rais  mwanamke lakini mama huyo ameisha waondolea  mashaka hayo na ndio maana mara kwa mara amekuwa akisema kuwa anaweza  na kweli  amaweza`` alisema Mizengo Pinda 

 Kwa upande wake Padri  Filibert Baligwa aliwaomba Watanzania  wawaombee  viongozi wa sasa walioko madarakani ili waweze kuongoza nchi kwa upendo na amani ili tuweze kupata manufaa ya nchi kwa wakati huu na wakati ujao 


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi,Beda Katani.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages