
Na Walter Mguluchuma KTPC, Sumbawanga.
JESHI la polisi mkoani Rukwa limefanikiwa kuwakamata watu 30 Katika operesheni maalumu iliyofanyika mwezi huu, wakituhumiwa kwa makosa tofauti likiwemo la kumiliki shamba la bangi.
JESHI la polisi mkoani Rukwa limefanikiwa kuwakamata watu 30 Katika operesheni maalumu iliyofanyika mwezi huu, wakituhumiwa kwa makosa tofauti likiwemo la kumiliki shamba la bangi.
Kwamujibu wa taarifa iloyotolewa na kaimu Kamanda wa polisi mkoani humo, Theopister Mallya alisema kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakikabiriwa na makosa ya kuvunja na kuiba, wizi wa pikipiki huku wengine wakikutwa wanamiliki shamba lenye ukubwa wa heka moja na nusu wakiwa wamelima bangi.
Alisema kuwa Operesheni hiyo ilifanyika Katika maeneo tofauti ya mkoa huo ambapo Katika tukio la kwanza watu 15 waliokua wakijihusisha na vitendo vya kuvunja nyumba za watu na kuiba walikamatwa wakiwa na Mali za wizi pamoja na vifaa wanavyotumia wakati wakivunja.
Kaimu Kamanda Mallya alisema kuwa Katika tukio la pili watu watatu walikamatwa na piki piki tano za wizi zenye namba za usajili MC 596 CDL aina ya Star, MC 220 AXG aina ya Star, na MC 285 CMX aina ya King lion.
Alisema kuwa pikipiki nyingine ni zenye namba za usajili T 218 BSQ aina ya T- Better, pamoja na pikipiki isiyo na namba za usajili yenye Chasis namba MG 2A211B2zewb79630 na Injini namba kl157FM13J26038 aina ya Boxer.
Mallya alisema kuwa katika tukio la mwisho watu 12 walikamatwa wakiwa wanamiliki shamba la bangi hekari 1.5 pamoja na bangi kavu yenye uzito wa kg 25 wakiwa wamezihifadhi ndani.
Alisema kuwa watu hao wamekuwa wakiuza madawa hayo ya kulevya Katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Rukwa.
Alisema watuhumiwa wote hao wanashikiliwa na watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali utakapo kamilika.