WAPIGANA MSIKITINI KATAVI NA KUVUNJA CAMERA YA MWANDISHI.


Na Mwandishi Wetu KTPC,Katavi.

Mwandishi wa Habari wa chanel ten mkoa wa Katavi paskal Katona amevunjiwa kamera yake wakati akitimiza majukumu yake ya kazi.

Mwandishi wa Habari wa chanel ten mkoa wa Katavi paskal Katona amevunjiwa kamera yake wakati akitimiza majukumu yake ya kazi.

Kuvunjwa kwa Camera yake kumetokea baada ya kutokea vurugu kubwa katika eneo la msikiti wa Makanyagia Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Waadishi wa Habari Mkoa wa Katati,Ndg Walter Mguluchuma wakati akielezea namna ya tukio hilo jinsi lilivyotokea.

Mwenyekiti huyo anaeleza kuwa kufutia kutokea kwa vurugu kwenye msikiti wa makanyagio majira ya saa 12 jioni walipokuwa wakimtangaza umamu  msikiti wa makanyagio ndipo waumini walianza kupigana ambapo kuanzishwa kwa vurugu hizo kulipelekea kuvunjwa  camera ya mwandishi huyo.

Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Katavi kinalaani vikali kitendo cha aibu kilichofanywa na waumeni hao.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages