DIWANI MASUMBUKO KUWASILISHA HOJA KWA BARAZA LA MADIWANI UJENZI WA KIVUKO.



Diwani wa Kata ya Shanwe Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Hafidhi Masumbuko akizungumza na wananchi wa kata hiyo namna ya kutekeleza ujenzi wa miradi ya maendeleo.



Na Alex Ngereza KTPC,Mpanda.

Diwani wa Kata ya Shanwe Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Hafidhi Masumbuko amesema kuwa atahakikisha ujenzi wa kivuko kinachounganisha Kata mbili za Misukumilo na Kilima hewa kuwa zinajengwa haraka ili kurahisisha shughuri za maendeleo.

Diwani wa Kata ya Shanwe Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Hafidhi Masumbuko amesema kuwa atahakikisha ujenzi wa kivuko kinachounganisha Kata mbili za Misukumilo na Kilima hewa kuwa zinajengwa haraka ili kurahisisha shughuri za maendeleo.

Diwani huyo amesema hayo leo wakati anazungumza na wananchi wa kata ya Shanwe namna ambavyo amejidhatiti kupitia baraza la madiwani anakwenda na ajenda kuomba serikali kutenga fedha za ujenzi wa kivuko.

Ameleza kuwa kama kivuko hicho kitajengwa kwa wakati kitakuwa chachu ya maendeleo kwenye kata zote hizo pamoja na manispaa ya Mpanda  hasa kwenye Nyanja ya kibiashara ambapo watu watatumia kusafirishia mizingo.

“ nitakwenda kuhakikisha na jenga hoja ya kufanikisha hili kwa sababu kimekuwa kilio cha watu cha muda mrefu sana” amesema diwani huyo.

 Katika hatua nyingine Diwani huyo amewashukia vikali walio tafuna fedha za ujenzi wa Zahati  ziliozochangwa na wanachi kuzirudisha haraka kabla ya kuchukua hatua kali zan kisheria.

“Ujenzi wa Daraja hilo utasidia kuepusha madhira ambayo yamelipotiwa kwa mara kadhaa ya watoto kupoteza Maisha” amesisitiza Diwani.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara baadhi ya wananchi wamesema kuwa mara kadhaa kumekuwa na matukio mengi ya watoto kusombwa na maji kwenye mto wa kata ya Shanwe pamoja na Misukumilo.

Daniel Katigili amempogeza diwani kwa kuonesha juhudi za kuwasaidia wananchi kuondokana na kero hiyo ya muda mrefu huku akimwahidi kumuuga mkono kwa kila jambo ambalo atakuwa na nia ya kulifanya kwenye kata hiyo.

“nafikiri mimi wamepita madiwani wawili kabla yako nimewaona nikiwa hapa sijapata diwani mwenye maneno ya kuwafariji wakazi wake kama wewe Mh Diwani wa sasa …nafikiri Mungu atakusaidia.

Aidha Daniel alieza baadhi ya kero ambazo wanakabiliwa nazo kama wazee hasa kwenye ubovu wa miundomibu ya barabara,hivyo ukiwa mzee njia nzima utakuwa ni mtu wa kuaguka anguka.

Said Hassain amesema kuwa kwenye sekta ya michenzo na burudani anapaswa kuiangalia kwa makini maana ni sekta ya ambayo inauwezo wa kuajili vijana wengi.

Amesema licha ya kuajili vijana wengi inapaswa kutengenezewa mazingira mazuri ya vijana kutumia fursa hiyo vizuri.


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages