Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,Mwl Alexius Kagunze akionesha baadhi ya sehemu ya madawati 1200.
Na George Mwigulu KTPC,Mlele
Halmashauri ya wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi imekamilisha zoezi la utengenezaji wa Madawati 1200 kwa shule za Msingi na sekondari ili kuondokana uhaba wa madawati uliokuwa ukisababisha baadha ya wanafunzi kukaa chini wakati wa masomo.

Halmashauri ya wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi imekamilisha zoezi la utengenezaji wa Madawati 1200 kwa shule za Msingi na sekondari ili kuondokana uhaba wa madawati uliokuwa ukisababisha baadha ya wanafunzi kukaa chini wakati wa masomo.
Mwl Alexius Kaguze,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele ameyasema hayo jana ofisini kwake wakati kielezea namna ambavyo halmashauri yake imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa maagizo ya serikali.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa mchanganuo wa ugawaji wa madawati hayo utakuwa madawati 700 kwa shule za msingi ikiwa pamoja na madawati 500 yatakayo pelekwa shule za sekondari.
Sambamba na kukamilika kwa kazi hiyo ya kutengeneza madawati alisema kuwa kama halmashauri inayo wajibu wa kuhakikisha inatengeneza mazingira bora ya mwalimu pamoja na mwanafunzi yatakayo chochea kiwango cha ufaulu kupanda kila mwaka.
" kukamilika kwa utengenezaji wa madawati haya ni mwendelezo wa juhudi unazofanya kama halmashauri za kuhakikisha mazingira ya utoaji elimu yanakuwa bora zaidi...hii ni siri ambayo inatufanya kwa miaka mitano mfululizo kushika nafasi ya kwanza kimkoa na kuingia kumi bora kitaifa kwenye matokeo yote ya mtihani ya kitaifa" alisisitiza Mwl Kagunze.
Mwl Kagunze ameweka wazi kuwa uandaji wa mazingira mazuri ya elimu unaendana pamoja na kuhakikisha watoto wote wanaofauli na kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari kuwa wanaripoti shuleni.
Rechal Kasanda,Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amepongeza juhudi za utengenezaji madawati pamoja na zoezi la kusimamia wanafunzi waliofauli kuwa wanakwenda shule.

Mkuu wa wilaya huyo ametoa maagizo ya kufanya ukarabati wa baadhi madawati yaliyoharibika ili yaweze kukaa kwenye hali nzuri zaidi ya kuendelea kutumika na wanafunzi madarasani.
Nao baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo Masingija Shigela amesema kuwa kama jamii a wilaya hiyo itaendelea kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali ili kuchochea maendelea kwenye sekta mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Shigela amesema kuwa wameamua kutumia nguvu kubwa kumuuga mkono Mkurugenzi wao kwenye sekta ya elimu kwani wana kiu kubwa ya kuona watoto wao wanafanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa.
Maria Paschal Mkazi wa Inyonga anaeleza kuwa elimu wanaiona ni mkombozi wa kuondoa umasikini wa fikra na kuwa elimu ni mwangaza wa maisha hayo,Hivyo wameamua kuwekeza elimu kwa watoto wao kwa kuwa ndio urithi pekee wanaowapatia watoto wao.
Aidha amempongeza Mkurugenzi mtendaji Mwl Alexius Kaguze kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kuhakikisha sio tu kwenye sekta ya elimu pekee anayoinua bali hata afya.