KAYA ZAIDI YA 40 MPANDA ZANUFAIKA NA MWENZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Diwani wa Kata ya Shanwe Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Hafidhi Masumbuko(wa kwanza kushoto) akiwa na baadhi ya watu aliowakabidhi bima za afya.

Na George Mwigulu KTPC,Mpanda.

Zaidi ya kaya arobaini za Kata ya Shanwe Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi zinazoishi kwenye hali ya mazingira duni zimenufaika na msaada wa mahitaji mbalimbali ya familia wakati wa mfungo wa mwenzi mtukufu wa Ramadhani.



Zaidi ya kaya arobaini za Kata ya Shanwe Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi zinazoishi kwenye hali ya mazingira duni zimenufaika na msaada wa mahitaji mbalimbali ya familia wakati wa mfungo wa mwenzi mtukufu wa Ramadhani.

Msaada huo wa mahitaji umetolewa jana kwa nyakati tofauti katika kaya hizo na Hafidhi Masumbuko ambaye ni Diwani wa Kata ya Shanwe,Manispaa ya Mpanda ambapo alieleza kuwa ameamua kufanya jitihada za kuwasaidia wananchi wenye uhitaji zaidi kwenye jamii kama sehemu ya kuonesha upendo kwao.

Diwani huyo alisema kuwa mahitaji aliyotoa kwa kila kaya ni pamoja na Kg 20 za Mchele,Unga wa sembe Kg 25,Sukari Kg 5,Chumvi Kg 2,Majani ya Chai yenye thamani ya fedha Tsh 25,000/= na Fedha Tsh 20,000/= kwa ajili ya kujikimu.

“ nimeona vema kufanya tendo hili la huruma hasa mwenzi huu wa Ramadhani pia nawakatia bima ya matibabu bure kwa watu sita wa kila kaya  yenye thamani ya fedha Tsh 30,000/= ili wapendwa wangu mtibiwe” alisema Masumbuko.

Alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kusaidia walengwa wa kaya ambazo zinawatoto yatima pamoja na wenye mahitaji maalumu ili nao wajisikie wako sehemu ya jamii inayowatambua na kuwajali.

“ nimetumia jumla ya kiasi cha fedha Tsh 5,600,000/=  kwa mahitaji haya lakini niko nagalia namna ya kuwasaidia angalau kila mwenzi…niwaombe wananchi wenzangu njooni tuwasaidie maana kutoa ni moyo na sio utajiri” alisisitiza Diwani huyo.

Masumbuko alisema  kuwa TASAF amewaomba kuagalia na kusaidia zaidi katika eneo hilo ikiwa na atatafuta mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) zitakazoweza kusaidia kaya hizo kutokana na kuwa idadi ni kubwa ya watu ambao wanahitaji kusaidiwa.

Kwa upande wa wanufaika wa mahitaji hayo Maulid Hassain Mkazi wa mtaa wa Kivukoni Kata ya Shanwe Manispaa ya Mpanda alimshukuru diwani kwa msaada na kuwaomba watu mbalimbali kujitokeza kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji maalumu.


“ mimi ni mzee sasa kwa kuwa nina miaka 70 na ninaishi na watoto hawa ambao ni yatima na wengine mama zao wametelekezwa na wanaume waliowapatia ujauzito,naishi maisha ya shida kuwalea lakini leo nimepata msaada” alisema Mzee Maulid.

Happy Oscar Mkazi wa Mtaa wa Kilimahewa Kata ya Shanwe Manispaa ya Mpanda  alisema kuwa kitendo kilichofanywa na diwani huyo kutoa zaidi ya milioni tano kutoka mfukoni kwake kuwasaidia hajawahi kukiona kwa madiwani wengine hapo awali kabla.

Alieleza kuwa kuna kila sababu ya vingozi wengine kujifunza kutoka kwa diwani huyo ambaye alimwita kuwa ni mtu anayependa kushirikiana na jamii inayomzunguka wakati wa shida na raha.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages