![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Comrade Juma Homera. |
Waadishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi wamepatiwa viwanja kila mmoja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi huku chama cha Waandishi wa Habari mkoani humo kimepatiwa kiwanja kimoja kwa ajiri ya ujenzi wa jengo la ofisi yao.
Waadishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi wamepatiwa viwanja kila mmoja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi huku chama cha Waandishi wa Habari mkoani humo kimepatiwa kiwanja kimoja kwa ajiri ya ujenzi wa jengo la ofisi yao.
Viwanja hivyo jumla ya 20 vimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Comrade Juma Zuberi Homera ofisini kwake ambapo amesema viwanja hivyo thamani yake ni milioni 40 na kuwa amevitoa kama sehemu ya kutambua mchango wa wanahabari wa kuutanga kwa anjia ya uhabarishaji.
Akikabidhi viwanja hivyo kwa wanahabari,Mkuu wa Mkoa wa huyo ameeleza kuwa ameamua kutoa viwanja hivyo ili kutekeleza ahadi yake aliyowahi kuitoa wakati wa kikao chake na wanahabari wa mkoa wa Katavi.
![]() |
Mwandishi wa Habari wa TBC Hosea Cheyo akiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati wa kukabidhiwa viwanja hivyo. |
'' nawapatia viwanja hivi wanahabari kwani vitawasaidia kujenga makazi yenu ya kudumu na kuwafanya mtekeleze majukumu yenu kwa weledi zaidi na mazingira salama...na ninapendekeza sehemu ya viwanja hivyo uitwe HABARI STREET" amesema Homera.
Pamoja na kutoa viwanja 20 kwa wanahabari hao,ameweza kutoa kiwanja kimoja kwa Chama Cha Waadishi wa Habari Mkoa wa Katavi (KTPC) kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya chama hicho ambachokimekuwa kiunganishi kikubwa baina yab waadishi wa habari na wadau walipo ndani na nje ya Mkoa wa Katavi.
![]() |
Zilper Joseph,Mwandishi wa Habari wa ITV Mkoa wa Katavi akiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati wa\makabidhiano ya viwanja. |
Homera ameweka wazi kuwa viwanja hivyo havihusiani kwa namna yoyote ya kumnyamazisha mwandishi wa habari kwenye kutekeleza majukumu yao kwa weledi bali waendelea kuibua changamoto zilizopo mkoani hapa.
Amesisitiza kuwa changamoto ambazo zimekuwa zikiibuliwa na waadishi wa habari mkoani hapa zimekuwa chachu ya kuisaidia serikali kutatua kero ambazo zinakuwa zinakabili wananchi.
Walter Mguluchuma,Mwenyekiti wa Chama Cha Waadishi wa Habari Mkoa wa Katavi amemshukuru Mkuu wa Mkoa huo,Juma Homera kwa kuwapatia waadishi wa habari viwanja hivyo na kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi wa chama hicho.
![]() |
Baadhi ya Waadishi wa Habari Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakati wa makabidhiano ya viwanja. |
Mwenyekiti huyo amesema kuwa ni viongozi wachache ambao wanatambua umuhimu wa vyote vya habari kama alivyofanya Mkuu wa Mkoa huyo kwa kuweza kutambua mchango wa wanahabari,Hivyo amewaomba na viongozi wengine wa nje ya Mkoa wa Katavi kuiga mfano huo wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Amewashauri wanahabari waliopewa viwanja hivyo kuhakikisha wanavitumia kujenga nyumba zao za kudumu na wasije wakajiingiza kwenye tamaa ya kuviuza kwani waadishi habari walio wengi vipato vyao ni vidogo,Endapo watauza viwanja hivyo huenda wakashindwa kununua viwanja vingine.
![]() |
Baadhi ya Waadishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa |
Mwanaid Waziri ambaye ni mwandishi wa Habari Mkoani wa Katavi ameone kama ni ndoto kuweza kumiliki kiwanja tena kwenye eneo la ndani ya Manispaa ya Mpanda.
Amewashukuru pia viongozi wa Chama Cha Waadishi wa Habari Mkoani hapo kwa ushirikiano wao mzuri na viongozi pamoja na wadau mbalimbali iliyopelekea kupatikana kwa viwanja hivyo.