![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Comrade Juma Zuberi Homera. |
Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera amemeagiza jeshi la Polisi hukakikisha linawakamata watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 18 watakao onekana wanazurula mitaani na kufanya biashara ndogo ndogo na kuuza vyuma chakavu kuwakamata na kuwaweka ndani na wazazi wao wakifike kuwakomboa na wawekwe ndani ili watowe maelezo kwa nini wanawatuma watoto wao kufanya biashara huku wakiwa na umri mdogo.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera amemeagiza jeshi la Polisi hukakikisha linawakamata watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 18 watakao onekana wanazurula mitaani na kufanya biashara ndogo ndogo na kuuza vyuma chakavu kuwakamata na kuwaweka ndani na wazazi wao wakifike kuwakomboa na wawekwe ndani ili watowe maelezo kwa nini wanawatuma watoto wao kufanya biashara huku wakiwa na umri mdogo .Homera ametowa maagizo hayo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Mji wa Mpanda .
Ameagiza kuwa mtoto yoyote yoyote ambae atakae aonekana akifanya biashara za kuuza bidhaa mbalimbali mitaani na kuuza vyuma chakavu wakamatwe mara moja na kuwekwa mahabusu na endapowazazi wao nao watajitokeza kwa ajiri ya kwenda kuwatowa nao watawekwa ndani na kisha watatakiwa wajieleze ni kwanini wanawatuma watoto wao kwenda kufanya biashara wakati wakijua kuwa ni watoto wao wanaumri mdogo .
Akiona tena kwenye meneo ya Mji wa Mpanda watoto wadogo wanaendelea kufanya biashara mitaani bila kukamatwa Mkuu wa polisi wa Wilaya ya Mpanda ajuwe kuwa ameshindwa kutimiza agizo la Mkuu wa Mkoa na mkuu huyo wa P olisi (OCD) atambue kuwa kuanzia siku hiyo atafute kituo kingine cha kufanyia kazi na si kwenye kwenye Wilaya ya Mpanda.
Amesema Mkoa wa Katavi hauwezi kupata kashifa ya watoto kutokwenda shule na badala yake wanafanya biashara mitaani.
Homera alisema haiwezekani watoto washindwe kwenda shule na badala yake wanakwenda kuuza vyuma chakavu na fedha hizo wanawapelekea wazazi wao.
Angekuwa na mamlaka angekuwa anawachapa vibokokabla ya kuweka mahabusu lakini polisi sheria hiyo inawaruhusu.
Serikali inaendelea kufanya shughuli za kupeleka maendeleo kwa wananchi na wao wazazi wanakuwa na tabia yao ya kuwatuma watoto wao kufanya biashara ya kuuza mayai.
Kumekuwa na tabia ya badhi ya watu watu kujifanya kuwa wanataka kununua bidhaa kwa watoto na badala wamekuwa wakiwaita hadi chumbani na kuwafanyia vitendo vya ubakaji .
Hapa ni mjini haiwezekani kuona watoto wanaendelea kufanya biashara mitaani watawakamata na wazazi wao watafikishwa Mahakamani.
Nae Mkazi wa Mtaa wa Majengo Josephina Joseph amesema kuwa agizo hilo la Mkuu wa Mkoa amelitowa kwenye wakati sasa kwani kemekuwa na wimbi kubwa katika mji wa Mpanda kwa watoto wadogo kufanya biashara mitaani muda wa masomo.
Juma Hussein Mkazi wa Mtaa wa Makanyagio amesema kuwa endapohatua za haraka hazitachukuliwa kuna uwezekano mkubwa wa tatizo la mimba za utotoni zikazidi kuongezeka kwa kasi kubwa.