![]() |
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Tabia Nzowa akifungua mafanzo ya kujea uelewa kuhusu mpango wa TASAF kipindi cha pili kwa viongozi,watendaji na wawezeshaji |
Na George Mwigulu,Katavi.
Wanasiasa nchini wametakiwa kutokuingilia mchakato wa utambuzi na uchambuzi wa kaya zilizo na mazingira duni ambazo zitaingizwa kwenye mpango wa kipindi cha pili ya awamu tatu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili kuepuka kaya zisizo na sifa kuingizwa kwenye mpango huo.
![]() |
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Zacharia Ngoma akifafanua masuala muhimu ya mpango wa TASAF. |
Wanasiasa nchini wametakiwa kutokuingilia mchakato wa utambuzi
na uchambuzi wa kaya zilizo na mazingira duni ambazo zitaingizwa kwenye mpango
wa kipindi cha pili ya awamu tatu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili
kuepuka kaya zisizo na sifa kuingizwa kwenye mpango huo.
Mpango wa TASAF wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ambao
umeanza kutekelezwa Feb 17/2020 na utakamilika mwaka 2023 utazifikia jumla ya
halmashauri 184 za Tanzania bara na visiwani ikiwa umejipanga kuhakikisha
vigezo na masharti vinazingatiwa kwa wanufaika wa mpango.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Zacharia Ngoma amesema hayo jana katika ukumbi wa St Mathias Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakati wa kikao kazi cha kujenga uelewa kwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo,viongozi,watendaji na wawezeshaji.
Ngoma amesema wapo baadhi ya madiwani ambao ni wanasiasa wamekuwa wakikusanya watoto na watu wenye uhitaji na kuwaweka katika mapagala ya majumba huku wakitumia nafasi zao kushawishi wawezeshaji wawakute huko kwa ajili ya kuwasajili kwenye mpango.
Kitendo hicho ambacho hakikubaliki kinazorotesha vigezo na
masharti ya kuwapata wanufaika wa TASAF na kuondoa uhalali wao wa kuwa sehemu
ya mpango wa uhawilishaji.
“viko vigezo vya kuzitambua kaya masikini,pamoja na vigezo vyako
lakini wananchi wenyewe wataweka vigezo vya kwao wenyewe kwa ajili ya kuitambua
kaya ipi inahali duni.Kwahiyo tuwaachieni wananchi wafanye kazi wenyewe”
alisema Ngoma.
Amesisitiza Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtedaji huyo “waheshimiwa
tukiliingilia zoezi hili mwisho wa siku tutakuja kuambiwa tumeingiza kaya
zisizo na sifa.Kwahiyo tafadharini sana tuwaache wasimamizi wasimamie zoezi hili
kwani watawaogoza wananchi kwa weledi na wanajamii wenyewe wazichagua kaya
ambazo kweli zinasitahili.Hivyo tusiingilie zoezi”.
Vilevile ameeleza kama watazichangua kaya zenye sifa zinazositahili itakuwa sifa kwa wanasiasa hao itakayowarahisishia kwenye uchanguzi ujao wa mwaka 2025 kuweza kuchaguliwa tena kuongoza kuliko kuingiza watu wasio na sifa na kusababisha wanakijiji kulalamika.
![]() |
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kujenga uelewa kuhusu mpango wa TASAF kipindi cha pili kwa viongozi,watendaji na wawezeshaji. |
Kwa kutambua mchango wa madiwani aliwaomba kuendelea kuhamasisha
wananchi kujitokeza kwenye vikao mbalimbali ili kuweza kupatiwa elimu zaidi juu
ya mpango huo kwani itasaidia kuepuka kuwa sehemu ya kutoa malalamiko kila
wakati yasiyo na tija.
Judith Woiso,Afisa Ufuatiliaji TASAF akitoa mafunzo hayo amefafanua kuwa mpango wa TASAF kipindi cha pili cha awamu ya tatu umejielekeza kwenye sehemu za mpango wa uhawilishaji ruzuku kwa kaya zenye watoto,kaya zenye wenye uelemavu na kaya zenye watoto wa kutimiza masharti ya elimu na afya.
![]() |
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mafunzo ya TASAF yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Nsimbo yaliyofanyika katika ukumbi wa St Mathias Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi. |
Aidha sehemu zingine za mpango ni kujenga uelewa kwa jamii kuhusu TASAF kupitia maonesho,mikutano ya jamii,nyombo vya habari,kushughurikia malalamiko ya walengwa,kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa shughuri za mpango pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wa ugani na kamati za usimamizi za jamii.
![]() |
Baadhi ya maofisi kutoka TASAF wakisikiliza mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa St Mathias Manispaa ya Mpanda na kuandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo. |
Awali akifungua mafunzo hayo ya siku tano Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Tabia Nzowa ametoa ushauri kwa washiriki wote kuwa wakati wa ziara wanazofanya za kikazi watenge muda wa kuongea na walengwa wa TASAF kwa kuwahamasisha kuanzisha miradi ya ujasiriamali ili kukuza vipato vyao.
Tabia amesema kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha wanufaika wanawakumbusha kuweka fedha za akiba kwa ajili ya kujikimu ili hata pale ruzuku inapochelewa au kusitishwa wawe wamejiwekea misingi bora.
![]() |
Baadhi ya wakuu wa idara ya Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye mafunzo ya TASAF. |
Naye Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Alex
Magesa amesema kuwa licha ya kuwa nyuma kwa asilimia 70 za kutekeleza mpango wa
TASAF wamejipanga kuhakikisha wanazifikia kaya duni na kuzisaidia.
Magesa ameweka wazi kuwa kati ya vijiji 54 vya Halmashauri ya
Nsimbo ni vijiji pekee 13 vilifanikiwa kufikiwa ikiwa ni asilimia 30 pekee ya
utekelezaji wa kwenye maeneo hayo.