MKUU WA MKOA MWAMVUA AWAAMBIA WAZEE SERIKALI ITAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumza na wazee wa Mkoa wa Katavi katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda. 


Na Paul Mathias KTPC,Katavi.

Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mlindoko amesema serikali itaendelea kutatua changamoto zinazo wakabilia wazee ikiwa ni sehemu ya kuatmbua Mchango wao kwa kazi kubwa walizozifanya katika Mkoa wa katavi na Taifa kwa ujumla.

Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mlindoko amesema serikali itaendelea kutatua changamoto zinazo wakabilia wazee ikiwa ni sehemu ya kuatmbua Mchango wao kwa kazi kubwa walizozifanya katika Mkoa wa katavi na Taifa kwa ujumla.

Akizungumnza na wazee wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa katavi katika kikao cha Kujitambulisha kwao Mkuu huyo wa mkoa amesema serikali imekuwa ikiendelea kuimalisha Miundo Mbinu kwa wazee ikiwemo suala la Matibu kwa kuwatengenezea Vitambulisho maalumu kwa wazee ili kuondoa adha wanayoipata katika suala la Matibabu.

Baadhi ya Wazee walio hudhuria kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwamvua Mrindoko.

Kwa upande wake Kiongozi wa wazee Mkoa wa katavi Thomasi Ngozi amesema wanamshuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa kujakwao kujitambulisha na kupata Baraka za wazee hao kwaajili ya kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa katavi.

"sisi wazee wa Mkoa wa katavi Tunakukalibisha sana katika mkoa wa Katavi wazee wa mkoa wa katavi niwakalimu"amesema Mzee Ngozi.

Kwa Upande wao baadhi ya wazee katika Manispaa ya Mpanda wamemuomba Mkuu huyo wa mkoa kuendelea kuimalisha huduma za jamii kwa wazee ikiwemo Matibabu,Upatikanaji wa Maji na miundo mbinu ya Barabara.

Katika hatua nyingine wamemuomba Mkuu huyo wa mkoa kuingilia kati Mgogoro wa ardhi uliopo baina yao na Jeshi la Wanachi wa Tanzania katika mkoa wa katavi kwa kuwa baadhi ya maeneo yao yamepolwa na Jeshi hilo hali ambayo wanakosa maeneo ya kuishi pamoja na kilimo kwaajili ya kuendesha Maisha yao.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda baina ya Mkuu huyo wa Mkoa na wazee wa Manispaa ya Mpanda kwa lengo la Kujitambulisha na kupata Baraka kwaajili ya kuanza kazi ya kuwatumikia wanachi wa mkoa wa katavi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages