Na Muhidin Amri KTPC,Mbinga.
SERIKALI imeipatia Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya ikiwa ni mkakati wa kuimarisha na kuboresha huduma za Afya hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wilaya ya Mbinga Juma Mnwele alisema, tayari wamepokea fedha hizo kutoka Serikali Kuu na wameshaanza kujenga Hospitali hiyo katika kijiji cha Kigonsera kata ya Kigonsera.
Mnwele amesema, ujenzi wa Hospitali hiyo utafanyika kwa awamu kulingana na fedha zitakazoletwa na Serikali na kwa kuanzia wataanza kujenga majengo ya vipaumbele kama jengo la wagonjwa wa nje(OPD) na maabara na kichomea taka na majengo mengine yataendelea kujengwa kulingana mapato.
Amesema, kwa kazi zilizofanywa na wananchi wa Kigonsera kusafisha eneo zimesaidia kuokoa fedha nyingi ambazo zitasaidia kuongeza majengo mengine ya kutolea huduma na kuwaomba wananchi hao kuendelea kufanya kazi za kujitolea katika mradi huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinda Desdelius Haule, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutao fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo na miradi mingine ya maendeleo inayokwenda kuharakisha kukua kwa uchumi.
Amesema, ujenzi wa Hospitali hiyo ni matokeo mazuri ya utendaji wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kuimarisha na kuboresha huduma za Afya kwa wananchi.
Katika kuunga mkono juhudi za Serikali Kuu,SerikaliI ya kijiji cha Kigonsera,imetoa zaidi ya ekari 35 za ardhi ili kujenga Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Emanuel Ngongi amesema, kwa kutambua changamoto walizokabiliana nazo kwa muda mrefu serikali ya kijiji kupitia mkutano Mkuu wa kijiji uliowajumuisha wananchi wote umeridhia kutoa ardhi iliyotengwa baada ya Halmashauri ya wilaya kuwa na wazo la kujenga Hospitali.
Ngongi amesema, wameamua kutoa ardhi hiyo bure ili kutekeleza mradi huo ambao unakwenda kumaliza changamoto ya huduma za afya kwa wakazi wa kijiji hicho ambao sasa wanalazimika kwenda hadi Hospitali ya Misheni Peramiho na Hospitali ya Rufaa Songea mjini umbali wa km 100
SERIKALI imeipatia
Mkurugenzi Mtendaji wa
Mnwele amesema, ujenzi wa
Amesema, kwa kazi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Amesema, ujenzi wa Hospitali
Katika kuunga mkono juhudi za
Mwenyekiti wa kijiji hicho
Ngongi amesema, wameamua
