WANANCHI WAMUOMBA RAIS SAMIA KUWATIZAMA VIONGOZI WA MIKOA YA PEMBEZONI MWANCHI WASIO WAADIRIFU.

 

Rais Samia Suluhu  Hassain

Na Mwandishi Wetu KTPC,Katavi.

Wananchi wa Mkoa wa Katavi wamemuomba rais Samia Suluhu Hassain kuwachunguza na kuwachukulia hatua baadhi ya viongozi wa nafasi ya uteuzi wa ofisi yake walio katika maeneo ya wilaya na mikoa ya pembezoni mwa nchi wanaofanya vitendo kinyume na maadili ya utumishi wa umma.

Hayo yametokana na baada ya rais Samia Suluhu Hassain alipomuhusisha Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika (Jina hakulitaja) kujihusisha ya migogoro ya ardhi kwa kujimilikisha hekali nyingi kwa matumizi yake binafsi huku akikwepa kulipa tozo za ushuru wa mazao yake.

Wakizungumza baadhi ya wananchi hao jana kwa wakati tofauti wa Wilaya ya Tanganyika na Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi walisema kuna dhana mbaya imejengeka miongoni mwa watumishi wa umma kutokuwajibika ipasavyo kwa kuwa wapo pembezoni mwa nchi na kuwa hawaonekani.

Zachari Chudu Mkazi wa Manispaa ya Mpanda alisema kuwa kauli ya rais Samia ya kuwataka wakuu wa mikoa na matibu tawala inaonesha yuko kwa ajili ya kuwatetea watu wananchi na nikauli ya kizalendo.

Zachari Chudu Mkazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Aidha alikiri kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa chanzo cha migogoro ambapo viongozi kama hao hawezi kusaidia jamii,Hivyo alimwomba rais kutafuta watu ambao waweuzo wa kusaidia jamii kuondoa migogoro.

Simba Hamis Mkazi wa Mkoa wa Katavi alisema kuwa viongozi wasio waadilifu ni kikwazo cha maendeleo ya nchi,Suala la kutumia nguvu zaidi ni kitendo kinachotumika kuwatisha ili kufanikisha masuala hiyo binafsi.

Mwananchi huyo amemwomba rais kuwatizama kwa umakini zaidi viongozi walio mikoa ya pembezoni mwa nchi kuwa baadhi yao wamekuwa wakutumia nafasi zao vibaya kwa masirahi yao.

Simba Hamisi Mkazi wa Mkoa wa Katavi.

Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi,Jesca Mbogo amempongeza rais kwa uteuzi aliofanya kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala hivyo aliwaomba wateule hao wakafanye kazi ya kumsaidia kazi na sio kuwa sehemu ya migogoro.

Kauli ya rais imeonesha dhamira ya dhati ya kuwasaidia wananchi katika kutatua migogoro ya wananchi ya ardhi kwa mkoa wa Katavi ambapo umekuwa kero kubwa kwao.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi  Jesca Mbogo.

Awali jana rais Samia Suluhu Hassain akiwaapisha makatibu tawala wa mikoa Ikulu Chamwino Jijini Dodoma aliwataka wa Kuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa kutokuwa sehemu ya migogoro ya ardhi kwa wananchi.

Alisema kuwa licha ya serikali kufanya juhudi kubwa ya kumaliza migogoro hiyo lakini bado ni migogoto ni mingi inapaswa kushuhurikiwaa na kuondosha uwonevu huo.

“ hatutamvumilia RAS na RC anaye jiingiza kwenye migogoro ya ardhi.atakaye ingia kwenye mkoa na akakuta ardhi ya watu wenyewe wapo akajimilikisha na kuitumia yeye huku akiwaacha watu wanalalamika.umepelekwa kwa kazi maalumu usiende kujishirikisha kwenye mgogoro wa ardhi” alisema rais Samia.

Rais alisisitiza “ kulikuwa na mgogoro moja huko wilaya ya Tanganyika kule,DC kaenda kajimilikisha maheka kadhaa na kalima Mungu kwa mwitikia…anatakiwa kulipa kodi ya mazao halipi,sasa DC huyu unamwacha wa nini?”.

Awali jana rais Samia Suluhu Hassain akiwaapisha makatibu tawala wa mikoa Ikulu Chamwino Jijini Dodoma aliwataka wa Kuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa kutokuwa sehemu ya migogoro ya ardhi kwa wananchi.

Alisema kuwa licha ya serikali kufanya juhudi kubwa ya kumaliza migogoro hiyo lakini bado ni migogoto ni mingi inapaswa kushuhurikiwaa na kuondosha uwonevu huo.

“ hatutamvumilia RAC na RC anaye jiingiza kwenye migogoro ya ardhi.atakaye ingia kwenye mkoa na akakuta ardhi ya watu wenyewe wapo akajimilikisha na kuitumia yeye huku akiwaacha watu wanalalamika.umepelekwa kwa kazi maalumu usiende kujishirikisha kwenye mgogoro wa ardhi” alisema rais Samia.

Rais alisisitiza “ kulikuwa na mgogoro moja huko wilaya ya Tanganyika kule,DC kaenda kajimilikisha maheka kadhaa na kalima Mungu kwa mwitikia…anatakiwa kulipa kodi ya mazao halipi,sasa DC huyu unamwacha wa nini?”.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages