Emmanuel Macron:Rais wa Ufaransa sio wa kwanza kushambuliwa kwa njia hiyo
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amepigwa kofi usoni wakati wa ziara rasmi ya kusini mashariki mwa Ufaransa.
Kwenye video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Bwana Macron anaonekana akitembea kwenda kwa kizuizi katika safari ya kwenda Tain-l'Hermitage nje ya jiji la Valence.
Mwanamume anampiga kofi bwana Macron usoni kabla ya maafisa kuingilia haraka. Rais, wakati huo huo, anakimbizwa kupelekwa eneo salama.
Wanaume wawili wamekamatwa kufuatia tukio hilo, kulingana na vyombo vya habari vya Ufaransa.