WAKULIMA WA MPUNGA KATAVI KUANZA KUNUFAIKA NA MBEGU ILIYOBORESHWA

Na Nkungu Haruna J-KTPC,Katavi.

Wakulima wa zao la mpunga mkoani Katavi wanatarajia kuanza kuvuna mavuno mengi kuanzia msimu ujao wa kilimo baada ya majaribio ya mbegu mpya ya mpunga ya SARO-5 kuonyesha matokeo mazuri. 

Wakulima wakivuna mpunga katika shamba la mfano (shamba darasa) katika kijiji cha Mwamkulu. Shamba hilo ni moja ya mashamba ya mfano yaliyopandwa mbegu ya mpunga iliyoboreshwa ya SARO-5, Katika mradi wa CARI-EA unaotekelezwa na shirika la ADP Mbozi kwa kushirikiana na wadau. Mbegu hiyo inatajwa kuwa na mavuno mara dufu kama ikilimwa kwa kufuata kanuni bora za kilimo.











Wakulima wa zao la mpunga mkoani atavi wanatarajia kuanza kuvuna mavuno mengi kuanzia msimu ujao wa kilimo baada ya majaribio ya mbegu mpya ya mpunga ya SARO-5 kuonyesha matokeo mazuri. 

Mbegu hiyo ilianza kufanyiwa majaribio mwaka huu katika shamba darasa lilipo kijiji cha Mwamkulu kilichopo manispaa ya Mpanda katika mradi wa CARI East Africa chini ya shirika la ADP Mbozi kwa kushirikiana na Nondo Investors na Matamba II Enterprises imeonesha kustahimili hali ya hewa ya mkoa wa katavi na kupokelewa vizuri na wakulima.

Edward Mwakagile ambaye ni mwakilishi wa shirika la ADP Mbozi akizungumza mara baada ya kutembelea shamba hilo kujionea matokeo ya mradi huo amesema lengo la kuleta mbegu hiyo ni kuwatoa wakulima wa mpunga mkoani Katavi katika kilimo cha mazoea ambacho hutumia gharama kubwa badala yake walime kilimo cha kibiashara ili waweze kunufaika.

Kwa upande wake Eric Damas aliyemwamkilisha Afisa Kilimo wa mkoa wa Katavi amewatoa wasiwasi wakulima kuhusu soko la mpunga na kuwashukuru wadau walioshirikiana katika kutekeleza mradi huo. Mradi huo CARI East Afica unatekelezwa Mkoani Katavi katika za Sibwesa, Mnyagala, Mwamkulu, Itenka na Kakese.


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages