RC MRINDOKO AMETOA WIKI 2 HALMASHAURI YA NSIMBO KUFUATILIA FEDHA ZAIDI YA MIL 71 ZA TOZO ZA USHURU ZILIZOSHINDWA KUWEKWA BENKI.




 

Na George Mwigulu,Nsimbo.

Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi imetakiwa kufuatilia na kusimamia mapato ya fedha ya zaidi ya milioni 71 ambayo haya kuwasilishwa benki na mawakala wa kukusanya mapato licha ya fedha hizo kukusanywa.


Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akitoa maagizo kwenye baraza la hoja la madiwani wa halmashauri ya Nsimbo.

Kifungu cha 50(5) ya LGFM kinataka mapato yote yanayokusanywa kupelekwa benki ndani ya siku za kazi ambapo kinyume na sheria hiyo menejimenti ilikusanya kiasi cha fedha Tsh 71,381,243.82 na kinaonekana kama madeni kwenye mfumo wa mapato bila kuwasilisha benki.

Mwanamvua Mrindoko ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliitaka halmashauri hiyo kutekeleza ufuatiliaji wa fedha hizo hapo jana kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Nsimbo wakati wa Baraza la hoja la madiwani la halmashauri hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Mohamed Ramadhani akitoa maelezo ya hoja za mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali  namna ambavyo wamezishuhhurikia kuzimaliza.

Mkuu wa Mkoa huyo akitoa maagizo hayo aliitakaTaasisi ya Kupambana na Kuzia Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi kufuatilia fedha hizo,akibainisha kuwa kitendo hicho ni aina nyingine ya ubadhirifu wa fedha za uuma.

“kama fedha zimekusanywa na kumbukumbu zinaonesha fedha zimekusanywa je kwanini hazipelekwi benki na zinakwenda wapi?” alihoji Mrindoko.

Katika kushughurikia tatizo hilo,Mkuu wa Mkoa huyo aliiomba Takukuru kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa haraka zaidi kabla ya tarehe 30,June,2021 na kuhifadhiwa benki sambamba na kufanya uchunguzi wa kubaini mwanya ambao watu wanatumia kuiba fedha hizo.

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi waliohudhuria kwenye baraza la hoja.

Vilevile alisema uchunguzi huo unatakiwa kubaini ni kwanini suala hilo linajirudia mara nyingi kwani kunauwezakano wa wakusanya ushuru ndani yake wako watu waliojipenyeza aidha watumishi au wenye mamlaka wanaotumia njia hiyo kwenda kwa wakusanyaji na kufanya ubadhirifu kwa pamoja.

Aidha aliipongeza halmashauri ya Nsimbo kwa kupunguza hoja 23 kati ya hoja 49 za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali,ambapo zaidi ya asilimia 50 zimeshafutwa huku akiwaomba kuendelea kupunguza hoja hizo ndani ya wiki nne ikiwa pamoja na kudhibiti kutengeneza hoja zingine zisitokee mpya.

Waheshimiwa Madiwani wa halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye baraza la hoja.

Mkurugenzi Mtedaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Mohamed Ramadhani  akitolea ufafanuzi wa fedha mil 71 alisema fedha hizo ni deni la muda mrefu,ambapo tangu anahamia katika halmshauri hiyo mwaka 2018 alikuta deni la zaidi ya mil 200 ambapo amefanya kazi kubwa kuhakikisha fedha zinapatikana.

Mohamed alifafanua halmashauri ya Nsimbo kuanzia Mwezi Julai,2020 wamebadilisha mfumo wa kukusanya mapato ili kuondokana na watu kukusanya mapato na fedha kubaki nazo mkononi.ambapo mfumo huo unamruhusu mkusanyaji wa mapato kutumia njia ya mitandao ya simu kulipa fedha ya serikali ndani ya masaa 24.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Halawa Malendeja alisema maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wameshayapokea na kama halmashauri wanajipanga kuhakikisha kila mmoja anasimama kwenye nafasi yake ili kuhakikisha kila ishara itakayowezaa kutengeneza hoja hapo baadaye wataishughurikia mapema pamoja na kumaliza hoja zilizopo 23.

Baadhi ya maofisa wa kamati ya ulizi na usalama na Takukuru wa Mkoa wa Katavi waliohudhuria kikao cha baraza la hoja la halmashauri ya Nsimbo.


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages