![]() |
| Waziri wa TAMISEMI,Ummy Mwalimu. |
Na Mwandishi Wetu KTPC,Mpanda.
Kuanzishwa kwa tozo mpya za kodi kwenye sekta ya mafuta na mitandao ya simu nchini imeelezwa kuwa ni ubunifu ulio na tija utakaofanikisha kamilisha ujenzi wa miradi ya maendeleo mbalimbali ya serikali.
Ubunifu huo uliofanywa na serikali ni mpango unaowakubusha wananchi kutambua kuwa ujenzi wa taifa lao utajengwa na wao mwenyewe na sio kwa kutegemea zaidi misaada ya nje ya nchi.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI)
,Ummy Mwalimu alisema hayo jana kwenye ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakati wa ziara ya siku nne mkoani hapo.
Ummy ameeleza kuwa ziara hiyo ni kwa ajili ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Katavi hususani kwenye maeneo ya elimu,afya na miundombinu ya barabara zinazosimamiwa na mamlaka wa wakala wa ujenzi wa barabara za mjini na vijijini(TARURA).
Aidha kusisitiza juu ya masula ya ukusanyaji wa mapato ndani ya halmashauri hasa kuona mapato ya ndani ya halmashauri yanayofanywa yanaelekezwa kutatua kero za wakazi wa Katavi hususani kwenye nyanja za afya,elimu ya msingi na sekondari pamoja na kuwawezesha wanaKatavi kiuchumi.
Vilevile ili kuweza kupata matokeo ya ziara hiyo amezungunza na sekretarieti ya Mkoa kwa ajili ya kuiwezesha,kuihamasisha na kuiimarisha itafanya kazi ya kumsaidia Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko na Waziri Ummy Mwalimu kwenye kusimamia shughuri za utawala na maendeleo katika halmashauri zote.
Katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo,Waziri huyo aliweka wazi kuwa kupitia tozo hizo mpya sasa wataweza kukamilisha ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa 186 ya shule za msingi na maboma 49 ya shule za sekondari Mkoani Katavi ikiwa zoezi hilo litafanyika nchi nzima kulingana na mahitaji ya mkoa wenyewe sambamba na kujenga shule moja kila jimbo ambapo fedha milioni 600 zitatumika kujenga shule hizo.
Waziri Ummy amesema kuwa zahanati jumla ya 900 zitajengwa nchini ambapo katika mkoa wa Katavi maboma 20 ya zahanati yatakamilishwa kujengwa na Zahanati 9 zitajengwa mpya ili kuhakikisha huduma ya afya zinaimarika zaidi katika utoaji wa huduma za matibabu na kuepusha wagonjwa kutembea umbali mrefu zaidi kutafuta matibabu.
Namna ambavyo tozo hizo zitakavyo saidia ni pamoja pia na kuongeza bajeti ya TARURA kutoka Milioni 600 hadi zaidi ya Bilioni 10,Fedha ambazo zitakwenda kujenga miundombunu ya barabara na kuimarika zaidi.
Ummy ameweka wazi pia kupitia wizara yake inakwenda kujielekeza zaidi kuweka kipaombele katika mikoa iliyo pembezoni mwa nchi ili kuhakikisha wanatoa zaidi rasilimali fedha na rasilimali watu kwa ajili ya maendeleo ya jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamua Mrindoko hapo awali akisoma taarifa kwa waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu,alisema mkoa wa Katavi unakabiliwa na changamoto za uhaba wa nisharti ya umeme ambayo haitoshi na kusababisha kasi ya shughuri za maendeleo kuwa chini.
Changamoto zingine ambazo mkuu wa Mkoa alisema ni upungufu wa watumishi kwa asilimia 43.9,Upugufu wa huduma ya maji ambapo iliyopo kwa sasa haikidhi mahitaji ya watumiaji wa Mkoa wa Katavi.
Aidha kwa sekta ya kilimo inakabiliwa na kukosekana kwa masoko ya uhakika ya mazao ya kilimo kama vile Mahidi na Mpungu hivyo kusababisha bei ya mazao haho kushuka zaidi na mkulima kushindwa kilimo kumkomboa kiuchumi.
Naye Mstaki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Haidary Summury alipongeza waziri hasa kwa mapango wake wa kuhakikisha wizara inatenga bajeti zaidi katika mikoa iliyo pembezoni mwa nchi kwani itachochea kasi zaidi ya maendeleo.
Summury amesema kuwa kwa muda mrefu mikoa kama Katavi imeshindwa kujikwamua zaidi kiuchumi kutokana na kuwa kama imesahaurika na serikali licha ya kuwa mikoa ya pembezo imekuwa ikabiliwa na changamoto nyingi za kijiografia,utawala na maendeleo.
Ubunifu huo umefanywa na serikali ni mpango unaowakubusha wananchi kutambua kuwa ujenzi wa taifa lao utajengwa na wao mwenyewe na sio kwa kutegemea zaidi misaada ya nje ya nchi.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI)
,Ummy Mwalimu alisema hayo jana kwenye ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakati wa ziara ya siku nne mkoani hapo.
Ummy ameeleza kuwa ziara hiyo ni kwa ajili ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Katavi hususani kwenye maeneo ya elimu,afya na miundombinu ya barabara zinazosimamiwa na mamlaka wa wakala wa ujenzi wa barabara za mjini na vijijini(TARURA).
Aidha kusisitiza juu ya masula ya ukusanyaji wa mapato ndani ya halmashauri hasa kuona mapato ya ndani ya halmashauri yanayofanywa yanaelekezwa kutatua kero za wakazi wa Katavi hususani kwenye nyanja za afya,elimu ya msingi na sekondari pamoja na kuwawezesha wanaKatavi kiuchumi.
Vilevile ili kuweza kupata matokeo ya ziara hiyo amezungunza na sekretarieti ya Mkoa kwa ajili ya kuiwezesha,kuihamasisha na kuiimarisha itafanya kazi ya kumsaidia Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko na Waziri Ummy Mwalimu kwenye kusimamia shughuri za utawala na maendeleo katika halmashauri zote.
Katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo,Waziri huyo aliweka wazi kuwa kupitia tozo hizo mpya sasa wataweza kukamilisha ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa 186 ya shule za msingi na maboma 49 ya shule za sekondari Mkoani Katavi ikiwa zoezi hilo litafanyika nchi nzima kulingana na mahitaji ya mkoa wenyewe sambamba na kujenga shule moja kila jimbo ambapo fedha milioni 600 zitatumika kujenga shule hizo.
Waziri Ummy amesema kuwa zahanati jumla ya 900 zitajengwa nchini ambapo katika mkoa wa Katavi maboma 20 ya zahanati yatakamilishwa kujengwa na Zahanati 9 zitajengwa mpya ili kuhakikisha huduma ya afya zinaimarika zaidi katika utoaji wa huduma za matibabu na kuepusha wagonjwa kutembea umbali mrefu zaidi kutafuta matibabu.
Namna ambavyo tozo hizo zitakavyo saidia ni pamoja pia na kuongeza bajeti ya TARURA kutoka Milioni 600 hadi zaidi ya Bilioni 10,Fedha ambazo zitakwenda kujenga miundombunu ya barabara na kuimarika zaidi.
Ummy ameweka wazi pia kupitia wizara yake inakwenda kujielekeza zaidi kuweka kipaombele katika mikoa iliyo pembezoni mwa nchi ili kuhakikisha wanatoa zaidi rasilimali fedha na rasilimali watu kwa ajili ya maendeleo ya jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamua Mrindoko hapo awali akisoma taarifa kwa waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu,amesema mkoa wa Katavi unakabiliwa na changamoto za uhaba wa nisharti ya umeme ambayo haitoshi na kusababisha kasi ya shughuri za maendeleo kuwa chini.
Changamoto zingine ambazo mkuu wa Mkoa amesema ni upungufu wa watumishi kwa asilimia 43.9,Upugufu wa huduma ya maji ambapo iliyopo kwa sasa haikidhi mahitaji ya watumiaji wa Mkoa wa Katavi.
Aidha kwa sekta ya kilimo inakabiliwa na kukosekana kwa masoko ya uhakika ya mazao ya kilimo kama vile Mahidi na Mpungu hivyo kusababisha bei ya mazao haho kushuka zaidi na mkulima kushindwa kilimo kumkomboa kiuchumi.
Naye Mstaki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Haidary Summury amepongeza waziri hasa kwa mapango wake wa kuhakikisha wizara inatenga bajeti zaidi katika mikoa iliyo pembezoni mwa nchi kwani itachochea kasi zaidi ya maendeleo.