UMMY  MWALIMU APIGA MARUFUKU KUHAMISHA WALIMU NA  WATUMISHI WA AFYA KWENYE MIKOA MINNE


Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi.

Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za  Mitaa Ummy Mwalimu amepiga marufuku huhamishwa kwa walimu na Watumishi wa Afya  wanao fanya kazi katika Mikoa ya Katavi ,  Kigoma  ,  Kagera.  Lind  na  Mtwara  mpaka hapo kuwe na watumishi wa kutoka sehemu nyingine ambao watakao chuo nafasi zao.

 Maagizo hayo ameyatowa kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa akiongea na  wananchi wa Halmashauri ya  Tanganyika,  na  Halmashauri ya  Nsimbo kwenye  Vijiji vya Ugala  Halmashauri ya  Nsimbo na  Halmashauri  ya Tanganyika .

 Alisema kuwa Mikoa hiyo ilikuwa na idadi ya watumishi wachache wa idara hizo mbili lakini Serikali  kwa sasa  imeelekeza nguvu kwenye Mikoa hiyo ili kupunguza tatizo hilo ambalo limekuwa likiikabili Mikoa hiyo  ambayo mazingira yake yameimalika

 Alimwangiza katibu Mkuu wa Tamisemi kuhakikisha kuwa walimu na watumishi wa Afya wanao  fanya kazi kwenye Mikoa ya Katavi ,   Kigoma , Lindi na  Mtwara  kutohamishwa mpaka hapo watakapokuwa wamewahamishia watumishi wengine kushika nafasi zao .

 Alisisitiza kuwa   endapo kuna mwalimu au mtumishi wa afya anae fanya kazi kwenye mikoa hiyo  ataondolewa pasipo kupeleka kwanza mtumishi mwingine wa kuchukua nafasi yake  atakuwa mkali kwa mtu atakae kuwa ameidhinisha uhamisho huo . 


Kuhusu wa Kurugenzi watendaji  wa Halmashauri ambao watateuliwa hivi karibuni kwenye mkeka ambao utakao toka  watambuekuwa watakuwa wanapimwa kwa jinsi ambavyo walivyofanya kazi ya  kutekeleza miradi ya maendeleo kutokana na fedha asilimia 40 ya mapato yao ya ndani .

 Waziri Ummy alibainisha kuwa  Wakurugenzi hao watakuwa wanapimwa kila baada ya miezi mitatu kwa jinsi walivyo kufanya mapato yao ya ndani  na jinsi walivyotumia fedha hizo kwa ajiri ya kufanyia shughuli za miradi ya maendeleo kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha fedha zinazokusanywa kwenye Halmashauri za mapato yao ya ndani zinatumika kwa ajiri ya kutatua kero za wananchi kwenye Halmashauri zao.
Alifafanua kuwa  Tamisemi wanampango wa kuangalia upya mgao wa fedha za barabara ili waweze kuzitowa kulingana na ukubwa wa Halmashauri kwani mgao walikuwa wamepanga wa kutowa milioni 500 kwa kila  haukuzingatia ukubwa wa maeneo hivyo mgao huo mpya utazingatia ukubwa wa Jimbo husika .

 Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mwanamvua Mrindoko alisema kuwa Mkoa wa Katavi unaupungufu wa watumishi wa karibu kwenye sekta zote zilizopo kwenye  Mkoa huu.

  A lisema licha ya kuwa na upungufu wa watumishi kazi zimekuwa zikifanywa na watumishi hao ambao walioko  kwenye  Mkoa wa Katavi  kama kawaida ambapo kwenye baadhi ya idara mtumishi mmoja amekuwa akifanya kazi  ambazo zinazotakiwa kufanywa na watumishi wawili .

Mbunge wa Jimbo la Nsimbo  Anna  Lupembe  alimshukuru Waziri wa Tamisemi  kwa  kuwahaidi wananchi wa Kata ya Ugala kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajiri ya kuanza ujenzi wa kituo cha afya ugala kitakacho saidia kuondoa vifo vya mama na mtoto.

 Alieleza  wananchi wa kata hiyo walikuwa wakilazimika kutembea umbali wa kilometa 76 kwenda kufuta huduma ya upasuaji  kwenye hospital  ya  Wilaya pindi mjamzito anapokuwa ameshindwa kujifungua  hali  ambayo imekuwa ikisababisha  wajifungulia njiani na wengine kupoteza maisha .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages