Katika mapambano ya magonjwa ya macho,Hosptali na vituo vya afya Mkoa wa Katavi vimenufaika kwa kupatiwa vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 121 ili kusaidia matibabu kwa wagonjwa.

Vifaa hivyo vilivyotolewa na shirika la TanzanEye International ni sehemu ya mpango wake wa kutokomeza magonjwa ya macho ambayo yameonekana kukithiri katika mikoa ya magharibi mwanchi.
Mkurugenzi Mtendaji Mkazi wa TanzanEye International,Ryner Linuma alisema hayo jana katika ukumbi wa Kituo cha Afya cha Mt,Aloyce Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakati akielezea malengo mahususi ya shirika hilo kwenye kusaidia jamii ambayo imeonekana kusumbuliwa na magonjwa ya macho.
Linuma alibainisha malengo ambayo wamefanikiwa ni kutoa vifaa tiba katika makundi mawili ambayo ni vifaa vya utoaji wa huduma za kibingwa ambavyo vilikwishaanza kutumika katika vituo vya kutolea huduma ya macho iliyofanyika 12-16 mwenzi Julai mwaka huu Mkoani hapa.

Vifaa tiba vingine ni vya upasuaji wa macho na viwezeshi vyake kwa lugha ya kitaalamu Surgucal equipment and consumables ambavyo vinahusisha pia vifaa vya kujikinga na maambikizi ya UVIKO-19 kwa wahudumu wa afya ya macho ambapo watapatiwa vitakasa mikono.
" ...vifaa hivi tumevitoa katika hosptali ya rufaa ya Mkoa wa Katavi,Kituo cha Afya Ilembo na Mt,Aloyce kwa Manispaa ya Mpanda,kituo cha afya Karema na Mishamo kwa wilaya ya Tanganyika,kituo cha afya Inyonga kwa wilaya ya Mlele,Hosptali ya halmashauri ya Nsimbo na Hosptali ya Tupindi kwa halmashauri ya Mpimbwe" alisema Linuma.

Katika hatua nyingine dhidi ya mapambo ya magonjwa ya macho,Shirika limempeleka mratibu wa macho Mkoa wa Katavi Dkt Japhet Chomba kwenda kupata mafunzo kwa vitendo Hosptali ya Ilembula.
Ikiwa sabambana na kusomesha wataalam wazawa ambao ni waajiriwa wa serikali na Jimbo Katoliki katika ubobezi wa utoaji wa huduma za macho ambapo ilipofika Februari,1 mwaka huu.Jumla ya wauguzi 16,wauguzi 12 kutoka vituo vya afya vya umma na wanne kutoka Kituo cha Mt Aloyce-Jimbo Katoliki Mpanda walichaguliwa kupelekwa chuo cha Mvumi-Dodoma kujifunza juu ya huduma za macho.

Aidha kuboresha miundombinu kwa kujenga jengo maalumu la huduma za macho pamoja na kuendeleza mahusiano baina ya sekta binafsi na sekta za umma katika utoaji wa huduma endelevu za macho katika mkoa.
Asikofu wa Jimbo Katoliki Mpanda Mkoa wa Katavi,Ezebius Nzigilwa aliwaomba wauguzi hao wa macho waliohitimu mafunzo maalumu waweze kufanya shughuli za utoaji wa huduma ya macho katika vituo vyao maana uhitaji wa huduma hiyo ni kubwa.
Asikofu Nzigilwa alifafanua kuwa anafahamu madkatari hawahudumii pekee kitaalamu bali kwa kutumia utu wa kujali,kuonesha upendo na kuwaelewa mahangaiko ya wagonjwa na kuwasaidia,Hivyo aliwaomba utoaji wa huduma wa kiwango cha juu.

" ninawaomba mtangulize utoaji wa huduma na sio masirahi kwa maana masirahi huwa yanakuja baadaye,kwani ukifanya vizuri utapata baraka kwa Mungu na masirahi mazuri yatapatikana" alisema Askofu Nzigilwa.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Dkt Mohammed Mpanjo alisema licha ya serikali ya mkoa wa Katavi kuwapongeza na kutambua kazi nzuri inayofanywa na TanzanEye International aliwataka wauguzi waliopata mafunzo kufanya kazi na sio kwenda kukaa.
Dkt Mpanjo alitoa maagizo kwa waganga wa kuu wa wilaya kutenga bajeti ya fedha maalumu kwa ajili ya ukarabati wa vifaa tiba ili viweze kufanya kazi kwa muda mreru na kufikia malengo ambayo wamejiwekea ya kuhudumia wananchi wa mkoa wa Katavi.