WAFANYABIASHARA MPIMBWE  WAOMBA TOZO ZA USHURU WA MAZAO YA KILIMO ZIPUMGUZWE.

Na George Mwigulu-KTPC,Katavi.
Wafanyabiashara wa mazao katika halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa  wa katavi wameomba kupunguziwa ushuru wa mazao ya mpunga ili kukidhi mahitaji ya kibiashara kulingana na gharama kubwa za maisha kuwa juu. 

Wakizungumza jana katika ukumbi wa shule ya sekondari Usevya halmashauri Mpimbwe wakati wa kuchangia hoja kwenye kikao kilichoitishwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na mbunge wa jimbo la Kavuu Geofrey Pinda,Wafanyabiashara walionesha wazi kutokuridhishwa na tozo za ushuru ambazo wanadai ni kandamizi kwao.

Elizabeth Joseph   mfanyabiashara wa zao la mpuga anadhibitisha kuwa tozo ya ushuru ya 3,500 kwa gunia moja la mpunga inayotozwa kwa sasa ni kubwa  zaidi kulingana na bei ya mazao hayo kuwa chini sokoni wakati wa kuyauza,ambapo huwafanya kupata faida ndogo inayowakatisha tamaa kuendelea na biashara ya mazao.

Mfanyabiashara Elizabeth alitoa mapendekezo ya kushusha tozo hiyo kutoka Tsh 3,500/= kwa gunia moja la mpunga inayotozwa kwa sasa hadi kufikia Tsh 2000/= kwa gunia moja kwani itawawezesha kuendelea kulipa ushuru huo kwa maendeleo ya halmashauri hiyo.

Abudulah Ismaili alisema kuwa halmashauri inapaswa kufanya uboreshaji wa mazingira ya kibiashara kwenye kilimo mazao kama sehemu ya utekelezaji wa kumwinua mfanyabiashara kiuchumi.

Alisisitiza serikali katika kutambua umuhimu wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika sekta ya kilimo inapaswa kufanya maboresho ya kodi,tozo za ushuru na ada za katika kilimo yafanyike yatakayo mnufaisha sio mkulima tu hata mfanyabiashara kwa sababu baadhi ya tozo hizo hutozwa  kwa mkulima na mfanyabiashara na kupunguza mapato yao.

Jojina kasamya ambaye ni mkulima na mfanyabiashara wa mazao alifafanua kuwa baadhi ya kodi na tozo zinazotozwa kwa wafanyabiashara zimekuwa zikiathiri ushindani wa mazao ya kilimo.

Ambapo hali hiyo husababisha wafanyabiashara kurudisha gaharana hizo kwa wakulima kwa kupunguza bei za mazao wanazolipa kwa wakulima.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,Catherine Mashalla akitolea ufafanuzi wa suala hilo alisema wapokea ombi hilo na watalifanyia kazi kwa ajili ya usitawi wa wafanyabiashara.

Aidha katika hatua nyingine mkurugenzi huyo alisema kiwango hicho cha kulipia shilingi 3,500/= kilijadiliwa na wadau wa mbalimbali katika kikao kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko na wao kama Halms hauri walikuwa wapokatika utekelezaji wa makubaliano ya kikao hicho kwa kufuata maazimio ya kikao hicho.

"sisi tupo katika utekelezaji wa maazimio ya kikao cha wadau kilichokubaliana kutozwa kiwango hicho cha fedha kwa wafanya biashara" alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la kavu Geofrey Pinda akitolea ufafanuzi suala hilo alisema kabla ya mwezi wa nane watakuwa wamekubaliana wadau kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa juu ya kuona namna ya kupunguza kiasi hicho ili wafanyabiashara hao waendelee kulipa tozo hizo kwenye kiwango cha chini ambacho ni sitahimilivu kwa wafanya biashara,

"nimeipokea changanoto hii lazima tushauriane namna ya kupunguza kiwango hicho ili wafanyabiashara waendelee kufurahia mazingira ya kibiashara katika halmashauri yetu" alisisitiza Geofrey.

Naibu waziri huyo ametoa wito kwa wafanya baishara kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini kuchangamkia fursa za kibiashara katika halmashauri ya Mpimbwe kwa lengo la kuitangaza halmashauri hiyo kwa fursa zilizopo katika halmashauri ikiwemo fursa za Kilimo,Viwanda na utalii Hali itakayosaidia kukuza wigo wa biashara na uwekezaji zaji katika halmashauri hiyo.

Wakizungumza jana katika ukumbi wa shule ya sekondari Usevya halmashauri Mpimbwe wakati wa kuchangia hoja kwenye kikao kilichoitishwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na mbunge wa jimbo la Kavuu Geofrey Pinda,Wafanyabiashara walionesha wazi kutokuridhishwa na tozo za ushuru ambazo wanadai ni kandamizi kwao.

Elizabeth Joseph   mfanyabiashara wa zao la mpuga anadhibitisha kuwa tozo ya ushuru ya 3,500 inayotozwa kwa sasa ni kubwa  zaidi kulingana na bei ya mazao hayo kuwa chini sokoni wakati wa kuyauza,ambapo huwafanya kupata faida ndogo inayowakatisha tamaa kuendelea na biashara ya mazao.

Mfanyabiashara Elizabeth alitoa mapendekezo ya kushusha tozo hiyo kutoka Tsh 3,500/= inayotozwa kwa sasa hadi kufikia Tsh 2000/= kwani itawawezesha kuendelea kulipa ushuru huo kwa maendeleo ya halmashauri hiyo.

Abudulah Ismaili alisema kuwa halmashauri inapaswa kufanya uboreshaji wa mazingira ya kibiashara kwenye kilimo mazao kama sehemu ya utekelezaji wa kumwinua mfanyabiashara kiuchumi.

Alisisitiza serikali katika kutambua umuhimu wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika sekta ya kilimo inapaswa kufanya maboresho ya kodi,tozo za ushuru na ada za katika kilimo yafanyike yatakayo mnufaisha sio mkulima tu hata mfanyabiashara kwa sababu baadhi ya tozo hizo hutozwa  kwa mkulima na mfanyabiashara na kupunguza mapato yao.

Jojina kasamya ambaye ni mkulima na mfanyabiashara wa mazao alifafanua kuwa baadhi ya kodi na tozo zinazotozwa kwa wafanyabiashara zimekuwa zikiathiri ushindani wa mazao ya kilimo.

Ambapo hali hiyo husababisha wafanyabiashara kurudisha gaharana hizo kwa wakulima kwa kupunguza bei za mazao wanazolipa kwa wakulima.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,Catherine Mashalla akitolea ufafanuzi wa suala hilo alisema wapokea ombi hilo na watalifanyia kazi kwa ajili ya usitawi wa wafanyabiashara.

Aidha katika hatua nyingine mkurugenzi huyo alisema kiwango hicho cha kulipia shilingi 3,500/= kilijadiliwa na wadau wa mbalimbali katika kikao kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko na wao kama Halms hauri walikuwa wapokatika utekelezaji wa makubaliano ya kikao hicho kwa kufuata maazimio ya kikao hicho.

"sisi tupo katika utekelezaji wa maazimio ya kikao cha wadau kilichokubaliana kutozwa kiwango hicho cha fedha kwa wafanya biashara" alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la kavu Geofrey Pinda akitolea ufafanuzi suala hilo alisema kabla ya mwezi wa nane watakuwa wamekubaliana wadau kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa juu ya kuona namna ya kupunguza kiasi hicho ili wafanyabiashara hao waendelee kulipa tozo hizo kwenye kiwango cha chini ambacho ni sitahimilivu kwa wafanya biashara,

"nimeipokea changanoto hii lazima tushauriane namna ya kupunguza kiwango hicho ili wafanyabiashara waendelee kufurahia mazingira ya kibiashara katika halmashauri yetu" alisisitiza Geofrey.

Naibu waziri huyo ametoa wito kwa wafanya baishara kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini kuchangamkia fursa za kibiashara katika halmashauri ya Mpimbwe kwa lengo la kuitangaza halmashauri hiyo kwa fursa zilizopo katika halmashauri ikiwemo fursa za Kilimo,Viwanda na utalii Hali itakayosaidia kukuza wigo wa biashara na uwekezaji zaji katika halmashauri hiyo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages