TAKUKURU KATAVI YATOA ONYO KWA MATAPELI WANAOJIFANYA MAAFISA WAKE.

Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Faustine Maijo 

Na George Mwigulu-KTPC,Katavi.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imewaonya na kuahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria matapeli wote TAwanaojifanya maafisa wa taasisi hiyo wanaochafua taswira na imani ya chombo hicho cha serikali kwa wananchi.

Hayo amesema jana Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi,Fautine Maijo alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji  kazi kwa kipindi cha mwenzi Aprili hadi Juni mwaka huu kwa waadishi wa habari ofini kwake ambapo licha ya kuelezea mafanikio makubwa waliowezakuyapata pia aliwaonya vikali watu wenye nia mbaya ya kuharibu taswira ya taasisi hiyo.

Maijo amesema kuwa kumekuwepo na wimbi la matapeli wanaojitambulisha kama wao ni maafisa wa Takukuru na hupiga simu kwa watu mbalimbali wakitoa maelekezo ya maagizo kwa watu hao ikiwa ni pamoja na kutakiwa kuripoti ofisi fulani ya Takukuru.

“ wanahabari,matapeli hao hutaka kuonana na wahusika na wamekuwa wakiwatapeli wananchi na baadhi ya watumishi kwa  namna nyingi” alisisitiza Maijo.

Kaimu wa Takukuru huyo licha ya kukemea vikali tabia hiyo na kuwataka waache mara moja aidha aliwaambia wananchi kutambua haki yao ya kuhoji utambulisho wa mtu yeyote anayejitambulisha kuwa ni afisa wa Takukuru.

Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi,Faustine Maijo akizungumza na wanahabari mkoani hapa wakati akiwasilisha taarifa kwa umma ya utendaji kazi wa robo nyingine ya mwaka.

Aidha alieleza mwananchi yeyote anayepewa wito wa kuitwa na maafisa wa Takukuru wanapaswa kujiridhisha kwa uhakika kuwa unakokwenda ni ofisi kweli za Takukuru na si kwingineko na endapo utapata mashaka jiridhishe na ofisi ya takukuru iliyokaribu sambamba na kupiga simu ya dharura 113 bure.

Vilevile alitoa wito kwa wananchi wote kutokubali kutapeliwa na kupaswa kutoa taarifa Takukuru ili mhalifu  huyo aweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwani ni kosa la kisheria kujifanya afisa wa Takukuru.

Katika hatua nyingine takukuru mkoa wa Katavi kwa kipindi cha mwenzi April hadi Juni,2021 imefanya kazi ya ufuatiliaji wa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo mitatu yenye jumla ya fedha Tsh 1,756,702,580/= na kubaini kuwepo kwa mapungufu machache ya kiutendaji na kuweza kutoa mapendezo  ya namna ya uboresaji.

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages