HALMASHAURI YA NSIMBO YATUMIA MBINU MPYA KUKUSANYA MAPATO YA NDANI ZAIDI YA BILIONI MOJA.



Mkurugenzi mtandaji wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Mohamed Ramadhani.

Na George Mwigulu,Nsimbo.

Halmashauri ya wilaya Nsimbo Mkoa wa Katavi imetumia mbinu mpya za ukusanyaji wa fedha za mapato ya ndani na kuvuka malengo kwa 132% ikiwa fedha hizo zitarejeshwa kwa wananchi kupitia miradi ya maendeleo.


Hayo alisema jana kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Nsimbo na Mkurugenzi Mtedaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo,Mohamed Ramadhani wakati akitoa taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi cha mwenzi Julai 2020 hadi Juni 2021 kwenye kikao cha baraza la madiwani.

Mkurugenzi huyo alieleza halmashauri hiyo ilikadiria kukusanya  mapato ya ndani fedha Tsh 823,982,639/- kwa mwaka 2020/21 ambapo kufikia 30,Juni mwaka huu imevuka malengo ya mwaka moja kwa kukusanya fedha zaidi ya bilioni moja.

Mohamed alisema licha ya kukabiliana na kushuka kwa uzalishaji wa zao la tumbaku,kusitishwa kwa vibali vya uvunaji wa mazao ya misitu,vitambulisho vya wajasiriamali,Mwitikio mdogo wa kununua viwanja vya makazi na biashara.

Vyanzo vya mapato kama ada ya matangazo,kodi ya viwanja ,ushuru wa mabango kuhamishiwa serikali kuu,matumizi ya force akauti katika utekelezaji wa miradi inayoathiri ushuru wa huduma na kupitishwa kwa sheria ya fedha ya mwaka 2017 ya kutotozwa ushuru wa mazao ya shamba ambavyo vyote hivyo vimeathiri ukusanyaji wa mapato ya ndani lakini mbinu mpya za ukusanyaji wa mapato zimetoa suruhisho.

Mbinu hizo ni pamoja na kuboresha minada ya Itenka,Mnyamasi,Ugalla na Sitalike,Kupandisha  ushuru wa vibali vya porini kutoka Tsh 5,000/- hadi Tsh 10,000/-,Kuanza kuwekeza katika kuanzisha masoko ya Songambele,Msaginya na Magula pamoja na kuanzisha stend ya Msanginya na Magula ili kuongeza wigo wa kukusanya mapato.

Aidha kusimamia sheria ya usafi wa mazingira kwa kuwatoza faini wasiotii sheria,kuimarisha doria ili kuzuia upotevu wa mapato na kuongeza ukusanyaji ikiwa na kuwekeza kwenye mazao ya biashara ya korosho na pamba ili kuongeza mapato ya halmashauri.

“ ndugu Mwenyekiti tumetoa vitambulisho kwa wakulima ili kubaini wafanyabiashara wa mazao wasio wakulima ambao walikuwa wanakwepa kulipa ushuru kwa kujifanya ni wakulima” alisema Mkurugenzi huyo.

Aidha Ramadhani alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21 baraza la madiwani ilikisia kupata fedha zaidi ya bilioni 22 ambapo hali halisi hadi kufika Juni,30 mwaka huu ilikuwa imepata fedha zaidi ya bilioni 13 sawa na asilimia 57 ya lengo la mwaka kwa mapato ya jumla.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Nsimbo Halawa Malendeja alisema kuwa halmashauri inahutaji zaidi kuongeza mapato ili iweze kusimama kwenye kutekeleza ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Malendeja alimwaomba mkurugenzi kupitia wataalamu wake kuendelea  kufanya tafiti na kubuni kilimo cha mazao mbalimbali na hasa ya kibiashara na kuimarisha sekta ya kilimo kwa ujumla ili kuwa sekta hiyo muhimili zaidi wa kukuza kipato cha halamashauri na wananchi wote.

Amesema Malendeja “ kuna maeneo mengi zao la mchikichi linalimwa kwa wingi,sasa sijajua kwanini kwenye halmashauri yetu halilimwi? ,Je kuna ugumu gani na ubaya gani kuwepo hapa?.niwaombe wataalamu wetu mtusaidie ikiwa pamoja na kuagalia hali ya hewa pamoja na sababu zote zinazotakiwa zizingatiwe ili zao hili liweze kulimwa


Vilevile amesema uanzishwaji wa zao la Mchikichi litasaidia wakulima kuwa wingo mpana wa kulima mazao mengi ya biashara yatakayosaidia kuufukuza umasikini kwenye halmashauri  ya Wilaya ya Nsimbo.

Kwa upande wa Lindila Matege,Diwani wa kata ya Kapalala alisema kuwa ili kuongeza ukusanyaji wa mapato ya halmashauri inatakiwa kuimarisha sekta ya ulinaji asili kwa kuhakikisha inaongeza tozo ya nta inayopatikana kwenye asili.

Alibainisha kuwa kwa sasa halmashauri hiyo haina tozo ya nta itokanayo na asali ikizingatiwa wafanyabiashara wamekuwa wakijipatia faida kubwa itokanayo na kuuza nta.

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages