| Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,Benjamin Kuzaga.. |
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mathias Sikazwe (68) Mkazi wa Kijiji cha Igongwe Kata ya Sitalike Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi amekamatwa akiwa na meno ya tembo mawili aliyoyahifadhi katika banda lakufugia mbuzi yenye thamani ya dola za kimarekani 20,000 kila moja.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi ,Benjamini Kuzaga mtuhumiwa huyo amekamatwa hapo jana majira ya saa saba usiku huko katika Kijiji cha Igongwe Kata ya Sitalike.
Kabla ya kukamatwa kwa mtumiwa Mathias Sikazwe,Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa mtuhumiwa huyo anamiliki meno ya tembo.
Kuzaga alieleza kuwa kufuatia kupatikana kwa taarifa hizo Jeshi La Polisi na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi walianza mara moja kufanya uchunguzi wa tukio hilo ili kuweza kumtia mbaroni mtuhumiwa.
Alieleza kuwa waliweza kufika nyumbani kwa mtuhumiwa na kufanya upekuzi kwenye makazi hayo na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa na meno ya Tembo mawili yenye uzito wa kilo 2.5 yakiwa ndani ya banda la kufugia mbuzi .
Alisema kuwa meno hayo ya tembo mawili thamani yake bado haija fahamika ni sawa na Tembo mmoja wenye thamani ya Dola elfu ishirini za Kimarekani.
Mtuhumiwa bado anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi na mara uchunguzi utakapo kamilika jalada litapelekwa katika ofisi ya taifa ya mashitaka ya Mkoa wa Katavi kwa ajiri ya kufanya utaratibu wa kumfikisha Mahakamani mtuhumiwa akaweze kujibu tuhuma zinazo mkabili .
Kamanda Kuzaga ametowa wito kwa Wananchi wanaojihusisha kufanya biashara haramu za magendo kama vile kuharibu rlasrimali za Taifa mfano ujangili waache mara moja kwani watambue tuu wakijaribu kufanya jeshi la polisi litawatia nguvuni .