![]() |

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu wakati wa kikao cha mwisho wa mwaka cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Mpanda kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo .
Amesema kuwa katika Halmashauri hiyo kuna upungufu wa walimu wa shule za msingi karibu katika shule zote zilizopo katika katika Manispaa ya Mpanda hali ambayo imekuwa ikiwafanya walimu kufanya kazi kubwa ya ufundishaji .
Idadi ya walimu ambao wamepungua ni walimu 767 kwenye Halmashauri hiyo ambayo ni idadi kubwa hivyo wanaiomba Serikali iendelee kuwapatia walimu ili kuweza kuondoa tatizo hilo la upungufu wa walimu .
Aidha Manispaa ya Mpanda inakabiliwa na tatizo la kutokamilika kwa miradi ya maendeleo kutokana na wananchi kuwa na mwitikio mdogo wa kuchangia shughuli za Maendeleo na kufanya miradi kutokamilika kwa asilimia mia moja .
Nzyungu alifafanua kuwa serikal imeisha towa maelekezo ya kujenga maboma ya shule na Zahanati na wakisha kamilisha ujenzi wa maboma Serikali hutowa fedha kwa ajiri ya kumalizia maboma yanayokuwa tayari kutokana na wananchi kutokuwa na mwitikio wa kuchangia kazi ya maendeleo Manispa wamekuwa wakilazimika kutumia fedha za mapato yao ya ndani kujengea maboma hayo ambapo fedha hizo zingeweza kutumika kwenye shughuli nyingine endapo kama wananchi wangejitolea.
Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidari Sumry aliwataka Madiwani wahamasishe wananchi wao kwenye Kata wanako toka ili wananchi hao waweze kushiriki katika kufana shughuli za kufanya kazi kwenye miradi ya maendeleo
Alisema kuwa mwaka huu Serikali imewaletea fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo kuliko hata walivyoomba hivyo nii vema madiwani madiwani waendelee kushirikiana na kusimia miradi ya maendeleo na matokeo yake yatazidi kuonekana zaidi .
Meya huyo wa Manispaa alieleza kuwa mwaka wa fedha uliopita wamejitahidi sana kukusanya fedha za mapato ya ndani na kuweza kuvuka zaidi ya asilimia mia moja kwa hivyo kwa mwaka huu wazidi kukusanya zaidi mapato hayo na kuyasimia vizuri .
Nae Diwani wa Kata ya Mwamkulu Alipi Katani aliomba kuwe na utaratibu wa maafisa kilimo kufika kwenye shule na kutowa elimu kwa wanafunzi ili wananchi wanao kuwa wanazunguka kwenye maeneo hayo ya shule waweze kujifunza utaalamu wa kilimo kwenye mashamba darasa ya kwenye shule hizo.
