![]() |
Baadhi wananchi walio hudhulia katika mnada wakiwa hawajachukua tahadhari ya kujilinda na UVIKO-19 |
NA HARUNA JUMA-KTPC,KATAVI.
Licha ya serikali kutangaza kuchukua tahadhari za kujikinga na UVIKO-19, wafanyabiashara ndogo ndogo (Wamechinga) na wateja wao katika soko la Majengo (Kapripointi) mjini Mpanda mkoa wa Katavi, wameonekana wakiendelea na shughuli zao bila kuchukua tahadhari yoyote ikiwemo kutovaa barakoa.
![]() |
Kwa mujibu Mwongozo wa udhibiti wa Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19) kupitia afua ya kuthibiti misongamano katika jamii bila kuathiri shughuli za kiuchumi, uliotolewa Julai 25,2021 na Wizara ya Afya, unazitaka halmashauri zote nchini ziainishe maeneo zaidi na kuangalia namna ya kupunguza msongamano ikiwa ni pamoja na kutumia viwanja vya mipira wa miguu au maeneo yoyote yaliyo wazi kwa ajili ya huduma za masoko au kushushia bidhaa.
Lengo ni kuwawezesha wafanyabiashara na wateja kuwa kwenye umbali unaokubalika na kuweka utaratibu kwa wateja kukaa umbali wa mita moja au zaidi wakati wa kupata huduma.
Kuweka utaratibu kwenye maeneo ya kuingilia ili kuhakikisha kila mteja na mfanyabiashara
Aidha mwongozo huo unamtaka kila anayeingia kupata huduma katika maeneo hayo awe amevaa barakoa au aelekezwe kununua barakoa bila shuruti , kila mwenye biashara aweke chombo chenye maji tiririka na sabuni na kila mara awaelekeze wateja wake kunawa kabla hawajaingia sokoni au dukani kupata huduma.
![]() |
Katika hatua nyingine iliamriwa kuwekwa maji tiririka na vitakasa mikono na kuvaa barakoa wakati wote kwenye maeneo yanayolazimika kukusanya idadi kubwa ya watu, ikiwemo masoko, hospitali, vituo vya mabasi, kumbi za mikutano na nyumba za ibada.
Hata hivyo hali imekuwa tofauti katika Soko hilo linalofanyika Jumapili ya kila wiki huwavutia wakazi wengi kutoka maeneo mbalimbali ya Mji wa Mpanda kwenda kupata mahitaji mbalimbali, ambapo imeshuhudiwa kutokuwepo kwa maji tiririka katika sehemu zote za kuingilia na kutoka na idadi kubwa ya watu imeshuhudiwa wakiwa hawajavaa barakoa.
Hali hiyo inajiri ikiwa tayari serikali imeshaanza zoezi la kusambaza chanjo katika mikoa mbalimbali nchini.