MANISPAA YA MPANDA WAPIGA MARUFUKU WAFANYA BIASHARA KUKESHA SOKONI

Meya wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Haidari Summury

Na Walter Mguluchuma-KTPC,Katavi .

Manispaa ya  Mpanda  Mkoani Katavi imepiga marufuku kwa wafanya biashara kufanya biasha usiku kwenye soko  la Mji wa Mpanda baada ya wafanya biashara kuanza kufanya biashara hadi usiku toka soko hilo lilipowekewa taa na badala yake wazingatie sheria za masoko .

Pia wamewaagiza watendaji wa Kata na Mitaa kuwaondoa kwenye maeneo yao wafanya biashara wanaofanya biashara kwenye maeneo ambayo siyo rasmi na endapo wafanya biashar hao hawata ondoka wataondolewa kwa nguvu na Halmashauri  hiyo .

Uamuzi huu wa  umetolewa hapo jana  kwenye kikao cha  Baraza la  Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mpanda kilichokuwa kinaongozwa na Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidari Sumry kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo .

Awali kabla ya uamuzi huu  Diwani wa Kata ya Kashaulili Magreti John alilieleza baraza hilo kuwa tangu soko kuu la mji huo walilipo wekewa taa wanafanya biashara wa soko hilo wamekuwa wakifanya biashara hadi usiku wa manane .

 Alihoji kuwa ivi utaratibu wa wafanya biashara kufanya biashara zao hadi usiku wa manane kwa  mji kama wa Manispaa wa Mpanda ukoje kwani yeye amekuwa akiona biashara zinaendelea hadi usiku na wengine kutokana na soko hilo kuwa na mwanga wamefanya kuwa ndio eneo la kufanyia mazungumzo muda wa usiku .

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael  Nzyungu alibainisha kuwa sheria za uwendeshaji wa masoko zipo wazi na nilazima kwa watu na wafanya biashara kuzifuata na kuzitii sheria hizo .

 Amefafanua kuwa muda wa kufunga masoko ni saa kumi na mbilli jioni  ila kwa kuwa  Manispaa ya Mpanda giza linachelewa kuingia wafanya biashara wanaruhusiwa kufanya biashara hadi saa moja  jioni hawawezi Kurusu kwa biashara kufanyika hadi usiku kwani mji wa Mpanda bado ni mdogo .

 Baraza hilo pia limetowa tamko la kuwaondoa wafanya biashara wadogo wote wanaofanya biashara kwenye maeneo yasiyo rasmi na kufanya biashara za kuuza mitumba na masoko yasiyo  rasmi hivyo Watendaji wa  Kata na Mitaa wafanye kazi ya kuwaondoa vinginevyo watakao kaidi wote wataondolewa kwa nguvu .

 Meya wa Manispaa Haidari Sumry alisema kuwa Halmashauri hawwezi kumwonea mtu hivyo wanaojua wafanya biashara kwenye maeneo ambayo siyo rasmi waondoke kwa hiyari yao na waende kwenye maeneo husika .

Aliwasisitiza madiwani hao kuwa jambo hilo lisiwe la baadhi ya madiwani kutaka   wafanya biashara hao wafanye biashara zao kiholela bali  tamko hilo limetolewa na madiwani wote sio wengine waonekana kuwa  wao ni wazuri na wengine ni mbaya.

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages