![]() |
| Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Benjamin Kuzaga akitoa taarifa kwa wanahabari mkoani humo ya kukamata majangili. |
Na Walter Mguluchuma-KTPC,Katavi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na kikosi maalumu cha kupambana na ujangili na uhalifu na Askari wa TANAPA wamefanikiwa kukamata meno ya tembo yenye uzito wa kilogramu 4.72 na silaha kali ya kivita aina ya AK 47 ikiwa na magazini moja yenye risasi 28 na nyama ya wanyama pori yenye uzito wa zaidi ya kilo 30.

Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Benjamin aliwaambia wandishi wa Habari kuwa katika msako huo waliofanya katika maeneo mbalimbali ya Mkoa kukabiliana na uhalifu na ujangili katika msako huu waliweza kukamata watuhumiwa tisa .
Katika tukio la agosti 22 majira ya saa tatu usiku huko katika maeneo ya mji mwema Kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda waliweza kumkamata Hamza Jonsia akiwa na nyara za Serikali vipande viwili vya meno ya tembo yenye uzito kiligramu 4.72 ambayo thamani yake bado haija fahamika.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuwa ametiliwa mashaka na baada ya kuwa amepekuliwa walimkuta akiwa na vipande hivyo vya meno ya tembo akiwa amehifadhi ndani ya begi la rangi nyeusi likiwa limeandikwa Bob marly
Katika msako huu uliendelea hapo mnamo Agost 23 majira ya saa nne usiku huko katika maeneo ya magogo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi waliwakamata watuhumiwa nane wakiwa na bunduki ya kivita aina ya AK 47 yenye namba UC 1988 ikiwa na magazini moja na risasi 28.
Kamanda Kuzaga alisema pia watuhumiwa hao walikamatwa na jino moja la tembo lenye uzito wa kilogramu 20 za nyama ya mnyama huyo na pia walikamatwa na pikipiki yenye Namba T 465AXL aina ya SunLg iliyokuwa imebeba nyama pori aina ya ngiri yenye kilogramu 35.

Kamanda Kuzaga amewataja watuhumiwa hao nane kuwa ni Fransis Thadeo Geremamano mkazi wa Kigamboni Manispaa ya Mpanda , Leonald Mtende Ngoyani (48) Mkazi wa Kawajense Manispaa ya Mpanda , Gabriel Milambo (42) Mkazi wa Kawajens, Phibart Libuma (30) mkazi wa Makazi ya wakimbizi Mishamo, Agustin Clavery Silasi (19) Mkazi za Sitalike na Peter Simon Matege (42) mkazi wa Shanwe.
Aidha Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi alitowa rai kwa wananci wanaojihusisha kufanya biashara haramu za magendo kama vile unaribifu wa rasilimali za taifa kwa kufanya vitendo vya ujangili uwindaji haramu kuacha na badala yake wajikite kufanya shughuli halali za kuwaingizia kipato.

Naye Afisa Mhifadhi anayesimamia kitengo cha himasheria na ulinzi wa kimkakati katika hifadhi ya Katavi (KANAPA), Lameck Matungwa alisema kuwa kama wahifadhi nchini wataendelea kufanya ushirikiano na wadau mbalimbali ili kutokomeza ujangili nchini.
Matungwa alibainisha kuwa kuendelea kuingizwa kwa siraha ndani ya hifadhi kunaleta madhara makubwa sio kwa tembo tu bali hata kwa wanyama wengi na kuathiri usitawi wa sekta ya utalii nchini ambapo imekuwa ikitegemea uwepo wa wanyama ambao huwa kivutio kikubwa kwao.
Vilevile alitoa wito kwa wananchi wanaozunguka hifadhi wasioneka kuwa ndio chanzo cha kuwakaribisha waharifu kwani miongoni mwa watu waliokamatwa na jeshi la polisi ni watu wanaoishi karibu na hifadhi.Hivyo wanapaswa kuwa sehumu ya watu wanaotoa taarifa mapema kwa polisi pindi wanapoona viashiria vya ujangili.
