![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko. |
Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi.
Waziri Mkuu Kassm Majaliwa anatarajia kuanza ziara ya siku tatu Mkoani Katavi ya kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa Mkoani hapa ukiwepo mradi wa ujenzi wa Bandaari ys Karema itakayo kuwa inatumiwa na Wananchi wa Tanzania na Nchi ya Kongo kwaajiri ya abiria na kusafirishia mizigo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko mbele ya Wandishi wa Habari ziara hiyo inatarajia kunza Agosti 25 hadi Agosti 27.
Amebainisha kuwa ziara hiyo ya siku tatu inalengo ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Mkoa huu
Ameitaja miradi miradi itakayo tembelewa na Waziri Mkuu Kassim Majali ni mradi wa bandari ya Karema inayoendelea kujengwa na inatarajia kukamilika hivi karibu ziara ya kutembelea Bandari hiyo itafanyika Agosti 25 ambayo ndio siku ya kwanza ya ziara yake
Amesema siku ya tarehe 26 atazindua kiwanda cha usindikaji wa pamba katika Kijiji cha Ifukutwa Wilaya ya Tanganyika na kisha ataelekea Mishamo kwenye makazi ya Mishamo ambako atakagua ujenzi wa kituo cha Afya cha Mishamo
Siku ya tatu ambayo ndio ya mwisho ya ziara yake Waziri Mkuu atatembelea kukagua ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi na kisha akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora atakagua baraba ya kiwango cha lami inayoanzoa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi hadi Mkoani Tabora .
Amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye maeneo yao kwa kujipanga barabarani kwa kuzingatia tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa Corona
Amesema kuwa kutokana hali iliyopo kwa sasa nchini ya tahadhari ya ugonjwa wa Corona kwenye ziara hiyo hakutakuwa na mikutano ya adhara .
Mrindoko amewaomba wakazi wa Mkoa huu kuwa watulivu kwenye kipindi hicho cha ugeni huu mkubwa na pia wananchi wajitokeze kwa wingi huku wakiwa wamepeana nafasi ya mita moja moja.
