MRADI WA FISH4ACP WAIMARISHA USAFI WA FUKWE ZIWA TANGANYIKA.

Mratibu wa Mradi wa FISH4ACP wa Mikoa wa Katavi,Rukwa na Kigoma Hashimu Muumin,Akizungumza na wanahabari pamoja na wananchi wa Ikola Wilaya ya Tangayika Mkoa wa Katavi  wa Mwaloni wa Ikola ziwa Tanganyika wakati akitamburisha mradi huo na malengo yake.

Na George Mwigulu,Tanganyika. 

Wananchi wa Mkoa wa Katavi wamehimizwa kuendelea kutunza na kusafisha fukwe za ziwa Tanganyika ili kulinda uhai wa viumbe vilivyo ndani ya ziwa ikiwa na kufanya uvuvi salama ili epuka kuwa sehemu ya kuchafua mazingira.


Kwa mujibu wa utafiti iliyofanywa na mradi wa kuimarisha uvuvi (FISH4ACP)ambao ni mpango wa  jumuiya ya nchi za Afrika,Karibiani na Pasifiki(OACPS) unaonyesha kuwa ziwa Tanganyika kina chake kimepungua kutokana na shughuri za kibinadamu zinazofanywa ndani na nje ya ziwa hasa zinazoambatana kuchafua fukwe na mwalo.

Hashimu Muumin,Mratibu  wa Mradi wa FISH4ACP katika mikoa ya Kigoma,Rukwa na  Katavi alisema hayo hivi karibuni katika kijiji cha Ikola walaya ya Tanganyika Mkoani hapa wakati akitaburisha mradi huo wa miaka mitano  uliombatana na kufisha fukwe na mwalo wa Ikola katika ziwa hilo.


Baadhi ya wananchi wa Ikola wakiwa katika mwaloni wa Ikola ziwa Tangayika kwenye jukumu la kusafisha mwalo huo,Zoezi hilo limeongozwa na mradi wa FISH4ACP.

Mratibu huyo amesema kuwa mradi wa FISH4ACP ni mpango  unaochangia usalama wa chakula na lishe ,ustawi wa uchumi  na uundaji wa kazi kwa kuhakikisha uimara wa uchumi,kijamii na mazingira wa uvuvi na minyororo ya thamani ya kilimo cha samaki.

Ameeleza kuwa FISH4ACP inataka kuongeza tija na ushindani wa uvuvi kumi na mbili na minyororo ya thamani ya ufugaji samaki katika nchi kumi na mbili za wanachama wa OACPS, kuhakikisha kuwa maboresho ya kiuchumi yanaenda sambamba na uendelevu wa mazingira na ujumuishaji wa kijamii.

Muumin amefafanua malengo ya kujitokeza kusafisha fukwe na mwalo wa Ikola kuwa ni mwendelezo wa wiki  ya kusafisha fukwe ambapo wanaungana na watu wengine wa ulimwenguni ili kuisafisha fukwe zetu ambazo zimeelemewa sana taka za plastiki ,taka ngumu ambazo zinaingia kwenye maeneo ya uvuvi.


Baadhi ya wananchi wa Ikola wakiwa katika mwaloni wa Ikola ziwa Tangayika kwenye jukumu la kusafisha mwalo huo,Zoezi hilo limeongozwa na mradi wa FISH4ACP.

Vilevile Kuongeza uelewa wa shughuli na matokeo ya mradi wa FISH4ACP kati ya hadhira ya Katavi na wadau wa mnyororo wa thamani wa Ziwa Tanganyika ikiwa na kuwasilisha matokeo ya uchambuzi wa mnyororo wa thamani (VCA), kushiriki wa uchaguzi wa  kimkakati kwa maafisa wa kiufundi katika Tawala za Mkoa wa Katavi ili kujadili na kupokea maoni yao juu ya uchambuzi.

Aidha wamefanikiwa kwenye  ukusanyaji wa taka za plastiki, magogo, nyavu za zamani, vyombo vya uvuvi vya zamani na vilivyoharibika, takataka zilizosambazwa kando ya pwani ya Ikola na njia za maji
Anthony Daudi kijana Mkazi wa Kijiji cha Ikola ambaye ameamua kujitokeza kufanya usafi katika mwalo wa Ikola ziwa Tanganyika pia amesema kuwa amewashukuru FISH4ACP  kwa mradi ambao umewaamsha kutoka usingizini kwa kutokutambua wajibu wao wa kusafisha fukwe na mwalo huo.

" ...wananchi madhara ya kuchafua fukwe na mwalo ni makubwa kwa kuwa yanasababisha upungufu wa samaki na kusababisha matatizo katika maeneo yetu ya mavuvi kwa sababu  taka zinazuia miale ya jua kuingia kwenye maeneo ya maji au vyanzo vya maji " Alisisitiza Mratibu huyo.

Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi,Donald Kusekwa akizungumzia juu ya mradi wa FISH4ACP na namna ambavyo kama serikali inashiriki katika masuala ya kuhakikisha fukwe na mwalo zinakuwa kwenye usafi

Afisa Uvuvi wa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Donald Kusekwa licha ya kushuru mradi huo amebainisha kuwa hali ya fukwe hapo awali za ziwa Tanganyika hazikuwa za kuridhisha na sasa wanaona mazingira niyakupendeza.

Kusekwa amesema hamasa iliyotolewa na mradi wa FISH4ACP kwa wananchi ni kubwa kwani umechangia wananchi kuona umuhimu wa kusafisha na kutunza fukwe na mwaloni kwa ajili ya faida yao na taifa,Hivyo kama serikali wataendelea kushirikiana na mradi huo.

Bi Salma Jumanne Mkazi wa Ikola akielezea namna ambavyo wamepokea mradi wa FISH4ACP kuwa umeleta hamasa ya kuhamsika kufanya usafi.

Salma Jumanne Mkazi wa Kijiji cha Ikola amesema kuwa kuishi kwa mazoea na kutokujali umuhimu wa kutokusafisha fukwe ilikuwa ni kikwazo kwao kujitokeza kusafisha,Kutokana na kutambua umuhimu wake kwa sasa hawatakubali kuwa nyuma kwa kushindwa kusafisha.

Amesisitiza kwa kuwaomba wananchi wote ambao wanaishi karibu na ziwa Tanganyika kupitia vikundi walivyoviunda kujitokeza bila kusita kufanya usafi kwenye fukwe na mwaloni ikiwa na kuwa mabalozi kila moja wa kukemea vitendo vya kuchafua mazingira.










Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages