
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa na mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Mkoa wa Katavi.
Na Mwandishi Wetu,KTPC Katavi.
Katika kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan la kutangaza rasilimali na Vivutio vya Nchi,Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Mhe.Sebastian Kapufi amewapeleka Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali Mkoani Katavi,kuzulu Hifadhi ya Taifa ya Katavi Jana Septemba 20,2021.
Akizungumza kusudi la kufanya hivyo Mbunge huyo amesema,kwa kutambua mchango wa Wanahabari anaamini kupitia Kalamu zao watatumia fursa hiyo kuitangaza Hifadhi hiyo iliyosheheni Vivutio vya kila aina vikiwemo Twiga,Tembo,Mamba,Viboko,Swala, Ndege wa kila aina n.k
"Sababu kubwa,Ndugu zetu hawa (Wanahabari) wanayo nguvu ya Kalamu,kwa kupitia Kalamu taarifa hizi za Utalii wa Ndani zitawafikia Watu wengi,kwa kupitia Kamera zao, taarifa zitawafikia Watu wengi. Lakini ni pamoja na kuunga jitihada,kuunga Mkono jitihada za Rais Wetu Samia Suluhu Hassan".

Akizungumza kwa niaba ya Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Katavi Bw.Walter Mwiguluchuma amemshukuru Mbunge huyo kwa nafasi hiyo adhimu huku akisisitiza kupitia Kalamu zao watahakikisha wainatangaza Hifadhi ya Katavi kwa kuwa ni miongoni mwa Hifadhi bora Afrika Mashariki yenye Vivutio vingi.
Mhe.Kapufi ameambatana na Waandishi wa Habari zaidi ya 15 wa vyombo mbalimbali Mkoani humo kwa ghalama zake mwenyewe ambapo wakiwa Hifadhini wamepata fursa ya kushuhudia makundi ya Wanyama na mandhali ya Hifadhi hiyo.