![]() |
| Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu,Richard Kayombo. |
Na George Mwigulu,KTPC Katavi.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewahakikishia wafanyabiashara wote nchi kuwa itaendelea kukusanya mapato ya kodi kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassain ya kukusanya mapato kwa njia ya maelewano kinyume na nguvu ili wafanya biashara waendelee kuiona TRA ni rafiki na sio adui wao.

Richard Kayombo,Mkurungezi wa huduma na elimu kwa walipa kodi wa TRA Makao Mkuu amebainisha hayo katika Ukumbi wa polisi,Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakati akifungua semina ya kuwajengea uelewa wa kulipa kodi kwa wafanyabishara mkoani hapa.
Semina hiyo ya siku moja ziliwasilishwa mada mbalimbali ikiwemo ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa mujibu wa sheria ya fedha ya mwaka 2021,Kupanua wigo wa kodi na kuleta usawa katika sekta ya kilimo kwa kuzingaitia sheria ya kodi ya ongezeko la thamani na mabadiliko ya sheria ya VETA 82.
Mkurugenzi huyo aliwasisitiza wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa kufuata taratibu na kutekeleza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati na wahakikishe wanapomuuzia mtu bidhaa wanampatia risti kwani inakuwa inasaidia makusanyo kupatikana kwa haki .
Kayombo alifafanua kuwa lengo la mamlaka hiyo sio kuwatoza watu faini wafanya biashara wanaoshindwa kulipa mapato kwa wakati hivyo kama wanataka wafanya biashara kuondokana na faini hizo wanatakiwa kutimiza wajibu wao kwa kulipa kodi kwa wakati .
Alibainisha kuwa wafanyabiashara wanapo lipa kodi kuna saidia serikali kuwaletea wananchi huduma muhimu za kijamii na ndio maana maeneo mengi yanayofanyiwa kazi na serikali yanayohusu kodi mbalimbali yanazingatia maoni ya wafanyabiashara
“ maboresho yanayofanywa na serikali kuhusu kodi yanazingatia maoni ya wafanyabiashara na yanawanufaisha kwa asilimia 70 hivyo kutokana na marekebisho hayo inaonesha jinsi gani serikali inavyofanya kazi zake kwa kushirikiana kwa ukaribu zaidi ndio maana wafanyabiashara wanayo haki ya kusikilizwa pindu wanapokuwa hawajaridhika na kodi” alisema Kayombo.
Isihaka Shariff, Afisa Msimamizi wa Kodi Idara ya elimu na huduma kwa mlipa kodi kutoka TRA akiwasilisha mada mbalimbali kwenye semina hiyo alisema hivi karibuni serikali imefanya maboresho ya sheria mbalimbali za kodi.
![]() |
| Afisa Msimamizi wa Kodi idara ya elimu na huduma kwa mlipa kodi,Isihaka Sharrif. |
Afisa huyo alisema baadhi ya maboresho hayo ni sheria ya kodi ya ongezeko la thamani ambapo mabadiko yamefanyika kwenye kifungu cha tatu yamefanywa kuwa kifungu kidogo cha kwaza,Vifungu vipya vimeongezwa 2,3 na 4 ambavyo vinaeleza kama VAT kwa bidhaa imelipwa Zanzibar kwa kiwango ambacho ni sawa na Tanzania bara ,basi bidhaa hiyo itachukuliwa imelipiwa kodi na haitatozwa tena kama itakaposafirishwa kwenda Tanzania bara.
Shariff alielezea kuwa ikiwa bidhaa imelipwa VAT Zanzibar kwa kiwango pungufu ukiliiinganisha na Tanzania bara,bidhaa hiyo ikihamishiwa bara,tofauti ya kiwango hicho cha VAT itakusanywa Tanzania bara.
“ naombeni mtambue ikiwa bidhaa imezalishwa Tanzania bara na kuuzwa kwa mtu aliyesajiliwa na VAT Zanzibar,kodi itakusanywa na TRA kwa niaba ya ZRB na kuirejesha kwa ZRB” alisisitiza Shariff.

Aidha serikali imefanya maboresho ya sheria ya kwa baadhi ya vitu baadhi ya vitu hivyo ni bidhaa mitaji , maboresho ya kusamehe vifaa vya kubebea maziwa , wamesamehe vifungashio vya madawa pia wamesamehe kodi ya simu za simu janja ili watanzania wengi waweze kunufaika na simu hizo .
Mwenyekiti wa Jumui ya Wafanya biashara Tanzania Tawi la Mpanda Amani Mahella aliwataka wafanya biashara wawe waaminifu kwa kufanya biashara zao pasipo kudanganya kwa lengo la kutaka kulipo kodi kidogo ambazo hazina uhalisia .
Kwani kitendo cha mfanya biashara kukwepa kulipa mapato ni kitendo kibaya sana na wala hakina faida bali kinakuwa kikimfanya mfanya biashara kuhatarisha biashara yake na ndio inaweza kumfanya asiendelee tena kufanya biashara kwani anaweza hata kukosa mtaji.

