NSSF KUNGANISHA MAKUNDI YA WAJASIRIAMALI KATAVI

 

 Benedick Joseph wela ni meneja wa NSSF Mkoa wa katavi amesema ofisi hiyo mkoa wa katavi kwa sasa imejikita katika kuhakikisha inayaunganisha makundi ya Wajasliamali, wachimbaji madini, wamachinga, wakulima, bodabado na makundi mengine lengo ni kuzifanya familia nyingi ziwe zimejiunga kwenye mfuko wa kijamii ambapo ameeleza kuwa vikundi 150 vimeanzishwa na kufunguliwa mfuko wa kijamii.




Aggrey james ni Afisa mafao Mkoa wa katavi anamuda wa mika 8 tangu amefika mkoa wa katavi mwazo alikuwa anatuma taarifa mkoa wa Rukwa lakini kwa sasa tangu wamepewa kutoa huduma za kimkoa wamekuwa na huduma bora na haraka kwa wanachama kwa kutoa Mafao yao kwa siku chache tofauti na mwanzo walikuwa wakichukua mwezi 3 hadi 4 kupata mafao yao kwa kutumia hundi wakati kwa sasa malipo yanafanyika kwa njia ya bank.




Juliana Mandege Afisa muongezaji michango ya wanachama Mkoa wa katavi huduma ambayo kama afisa wiki hii ya huduma kwa wateja anajivunia kutoa huduma ya Mafao kwa wanachama kwa muda mfupi na hata kabla ya siku 30 wanazowaeleza wananchama.


Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa katavi wakiendelea na majukumu ya kuhakikisha wiki ya wateja inaenda kwa mafanikio makubwa huku wakiendelea kuwaomba wananchi kujiunga na mfuko huo kutakana umuhimu wake kwenye jamii pamoja na familia moja moja


Lucy Peter mkazi wa Manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi amesema huduma zinazotolewa na NSSF kwa sasa zimekuwa zaharaka lakini zimeboreshwa tofauti nailivyokuwa awali walipokuwa wakifata huduma hizo mkoa wa Rukwa wanafurahia huduma hizo


 

 

 

 

 

 

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages